Wananchi wa Mtaa wa Luhende, Manispaa ya Shinyanga,
wamemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami
kutoka mjini Shinyanga kupitia Kata ya Ndala kuelekea Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Shinyanga kuongeza kasi ya kazi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na
kuondoa adha wanazokabiliana nazo.
Akizungumza na Gold FM, Mwenyekiti wa Mtaa wa Luhende, Msafiri Nadula, amesema kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi huo kumesababisha usumbufu kwa wananchi, huku shughuli za biashara katika maeneo yanayopitiwa na barabara hiyo zikiathirika kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kando ya barabara hiyo wamesema tangu kuanza kwa ujenzi wamekuwa wakikosa wateja kutokana na mazingira ya vumbi, mashimo na mabadiliko ya njia za kupita, hali iliyosababisha mitaji yao kudorora.
Wakazi wa maeneo hayo wameendelea kuunga mkono utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa utaleta maendeleo ya muda mrefu, lakini wameendelea kuiomba Serikali na mkandarasi kuhakikisha kazi zinafanyika kwa kasi ili kupunguza athari zinazowakabili kwa sasa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment