" MSANII CHAP CHAP HALI YAKE NI MBAYA ANAOMBA MSAADA WA FEDHA KWA AJILI YA MATIBABU

MSANII CHAP CHAP HALI YAKE NI MBAYA ANAOMBA MSAADA WA FEDHA KWA AJILI YA MATIBABU

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Taarifa kutoka kwenye chama cha waigizaji (TDFAA) Mkoa wa Shinyanga

Msanii wa nyimbo za utamaduni katika kikundi cha Sanaa Mkoani Shinyanga Arts Group, Bwana Fadhili Mungi jina maarufu Chap Chap anaomba msaada wa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.

Msanii Chap Chap mwenye umri wa Miaka 44 ni mkazi wa Msikamano kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga zaidi ya miezi miwili akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa kutokwa na usaha puani, maumivu makali ya kichwa , kutokwa na vipande vya nyama na maumivu mengine.

Taarifa hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa chama cha waigizaji (TDFAA) Mkoa wa Shinyanga Neema Philipo Mushi ambapo amesema kwa mujibu wa taarifa za madaktari anahitaji takribani shilingi Milioni Nne (4) ili aweze kufanyiwa upasuaji ambapo kwa sasa anaendelea kutumia dawa za kutuliza maumivu shilingi 98,000\= kila mwezi na kwamba miezi kadhaa amekuwa akiteseka.

Chap Chap anaiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia ilia pate matibabu kwani hana uwezo wa kifedha wa kufanikisha matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.

Chama cha waigizaji Mkoa wa Shinyanga kimeshaunda kamati itakayoratibu na kupokea fedha kwa mtu anayeguswa Namba ya simu 0747956257 na Mungu atakubariki.

Ofisi ya UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kupitia Mwenyekiti wake Bwana Jonathan Madete wameshiriki kikao cha pamoja na wasanii wa maigizo, Bongo fleva, Gospal, Dancers, Photographer, Videographer na waandishi wa habari kujadili namna ya kusaidia Chap Chap ili aweze kupata matibabu kwa uharaka.

Post a Comment

Previous Post Next Post