Mtu Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Daud kulwa Mwandu Mwenye
umri wa Miaka 25,Mkazi wa Bugweto kata ya Chamaguha amefariki
Dunia baada ya kugongwa na Gari kwenye Barabara kuu ya Shinyanga
Mwanza.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, ajali hiyo imetokea
majira ya saa Nne asubuhi Daud akiwa amebebwa kwenye usafiri wa
Baiskeli ndipo Gari hiyo ilipowagonga na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Wameeleza kuwa mwendesha baiskel Athuman Mtatiro mwenye umri
wa miaka 33,mkazi wa tambukareli aliyekuwa amempakiza Daud
ambaye kwa sasa ni marehemu amekimbizwa hospitali ya Manispaa ya
Shinyanga kwa ajili ya matibabu
Kufuatia ajali hiyo wakazi wa maeneo hayo wamelalamikia madereva
kuendesha mwendo kasi hali inayochangia ajali za mara kwa mara
ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt PIELINA
MWALUKO amethibitisha kupokea Mwili wa Marehemu huyo na
majeruhi mmoja ambaye amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
kamishina msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amelitaja gari hilo kuwa ni
aina Toyota Landcruser T.652 DST iliyokuwa ikitokea Mjini kuelekea
maeneo ya Ibadakuli ikiendeshwa na Sheikh Ismail Habib Makusanya.
Post a Comment