" WIKI YA SHERIA YAWANUFAISHA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ISELAMAGAZI

WIKI YA SHERIA YAWANUFAISHA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ISELAMAGAZI


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Iselamagazi iliyopo Mkoani Shinyanga wamejengewa uelewa kwa kupata elimu kuhusiana na Sheria mbalimbali zinazotumika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa elimu hiyo Januari 29, 2024 Mkaguzi kata wa kata ya Iselamagazi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Brighton Rutajama aliwataka wanafunzi wa shuke hiyo kujiepusha na makundi ya kihuni au kutojiingiza kwenye vitendo vya kihalifu kwani Jeshi la Polisi alitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Mkaguzi huyo aliwaelezea maana na  utofauti kati ya Sheria zinazoshughulikia makosa ya jinai pamoja na zile zinazoshughulikia na kesi za madai.

Aidha, wanafunzi hao pia walinufaika na elimu ya kutoa ushahidi Mahakamani pamoja na watu wanaotakiwa kutoa ushahidi mbele ya mahakama.

Toka Dawati la Habari Polisi Manispaa Shinyanga

 

Post a Comment

Previous Post Next Post