
Na Gift Mongi, Misalaba Media- Morogoro
Kamati ya kudumu ya bunge viwanda biashara kilimo na mifugo wametembelea mashamba ya miwa ya Mkulazi (Wilaya ya Kilosa) na Mtimbwa (Wilaya ya Mvomero) na viwanda vyake vya sukari.
Miongoni mwa mjumbe katika kamati hiyo ni mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ambaye pia alieleza dhumuni la ziara hiyo muhimu mjumbe wa kamati hiyo.
Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa ziara hiyo ilikuwa mahsusi kufuatilia uzalishaji wa sukari kwenye viwanda hivyo katika kipindi hiki cha mvua za El Nino zinazoendelea nchini.
Wajumbe wa kamati walijionea uharibifu mkubwa wa miundombinu uliosababishwa na mvua na kuzorotesha uzalishaji wa sukari.
'Ziara hii ni muhimu kwetu tumejionea uharibifu uliofanyika lakini pia tumepata angalau wasaa kuweza kuishauri serikali'alisema
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi akiwa katika Mashamba ya miwa ya kiwanda cha Sukari cha Mtibwa pamoja na wanakamati wenzake na watumishi wa shamba la Mtibwa.
Picha nyingine anaonekana Profesa Ndakidemi akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi (Katikati) na Profesa Sospeter Muhongo, mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo.
Post a Comment