Wanafunzi wa shule ya Sekondari Masekelo iliyopo Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kutojenga hofu kwa Askari Polisi hususani katika utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Rai hiyo imetolewa Januari 29, 2024 na Mkaguzi kata wa Kata ya Masekelo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Yasinta Bakari wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi shuleni hapo.
Alisema "Toeni hofu kwa Askari Polisi kwani wao ni wanajamii wenzenu kuweni na ushirikiano nao, toeni taarifa za uhalifu na wahalifu ili tuendelee kuwa salama sababu ulinzi na usalama ni wajibu wetu sote" alisema Mkaguzi Yasinta.
Mkaguzi huyo pia alipata fursa ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Polisi Jamii kwa wananchi pamoja na kutambua viashiria vya ukatili wa kijinsia sambamba na kumtambua mtu aliyefanyiwa ukatili na kumtambua aliyefanya ukatili na namna sahihi ya kumripoti kwenye vyombo vya sheria.
Toka Dawati la Habari Polisi Manispaa ya Shinyanga

Post a Comment