Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amewataka
wakazi wa wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho vya Uraia (NIDA).
Amesema vipo vikundi pamoja na baadhi ya wananchi
wamekuwa wakikosa fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa sababu ya kutokuwa na
kitambulisho cha Uraia (NIDA).
DC Mkude amehimiza wakazi wa Wilaya ya Kishapu
kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua
vitambulisho hivyo ili viweze kuwasaidia katika fursa mbalimbali zinazojitokeza.
Amesema vitambulisho vya Uraia (NIDA) 67864
vimesambazwa kwenye ofisi za watendaji wa kata katika Wilaya ya Kishapu ambapo
amesisitiza wananchi kwenda kuchukua vitambulisho vyao.
“Vitambulisho
hivi tumekuwa tukivisubiri kwa muda mrefu lakini sasa hivi tunaenda kwenye
matumizi makubwa ya vitambulisho hivi huwezi kufanya jambo lolote bila kuwa na
kitambulisho cha NIDA, sasa hivi hata mikopo wanasisitizwa kuwa na vitambulisho
hivi ili kupata mkopo sasa niwaombe wananchi wajitokeze kwenda kuchukua
vitambulishi vyao kwenye ofisi za watendaji wa kata”amesema
DC Mkude
Post a Comment