" INDONESEA KUSAIDIA TANZANIA KUZALISHA BIDHAA MBALIMBALI IKIWEMO ZA NGOZI ILI KUSAIDIA UKUWAJI WA UCHUMI.

INDONESEA KUSAIDIA TANZANIA KUZALISHA BIDHAA MBALIMBALI IKIWEMO ZA NGOZI ILI KUSAIDIA UKUWAJI WA UCHUMI.


Kufuatia Uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Indonesia unatajwa kuwezesha watanzania kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora ikiwemo viatu vya ngozi na kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi.

Balozi wa Indonesia nchini TRI YOGO JATMIKO amebainisha hayo Jijini Mwanza wakati akifungua mafunzo ya kutengeneza viatu vya ngozi vyenye ubora yanayotolewa na wataalam kutoka mataifa ya Indonesia na Ujerumani.

Balozi JATMIKO amesema kuwa dhamira ya Indonesia ni kuendelea kuijengea uwezo Tanzania pamoja na watanzania kwenye Nyanja mbalimbali ili kuwezesha Taifa kupiga hatua kwenye maendeleo kama ilivyo kwa Indonesia.

Mafunzo hayo yanayowashirikisha wazalishaji 25 wa bidhaa za ngozi kutoka mikoa mbalimbali nchini yanafanyika kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar-es-salaam(DIT) kampasi ya Mwanza

Mkurugenzi wa DIT kampasi ya Mwanza DOKTA ALBERT MMARI amesema ujio wa wataalam wa bidhaa za ngozi kutoka nchini Indonesia ni miongoni mwa matunda ya ziara ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN aliyoifanya nchini humo mapema mwaka huu.

Naye mwakilishi wa mkuu wa wilaya ilemela MARCO ISAKA amesema kuwa ujio wa wataalam hao utasaidia kukuza ujuzi wa watanzania kwenye Tasnia ya uzalishaji wa bidhaa za ngozi hususani viatu.

Kwa upande wao,wazalishaji wa bidhaa za ngozi wanaoshiriki kwenye mafunzo hayo wamesema yatawawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kumudu ushindani wa kibiashara kwenye soko la ndani pamoja na nje ya nchi.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post