Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amewaongoza waumini wa Dini hiyo kufanya usafi wa mazingira katika eneo la kituo cha Afya kambarage Mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ibada kuelekea kwenye maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad swala-lahu-alleyh wasallam
Sheikh
Ismail amesema kabla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad waumini wa dini ya kiislamu watashiriki kutoa
huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo misaada kwa wahitaji na kufanya usafi wa
mazingira katika taasisi za Umma ikiwemo kituo cha Afya kambarage.
Amesema
usafi ni sehemu ya ibada katika mafundisho ya dini ya kiislamu kimwili na kiroho,pamoja na mazingira ya
kuishi ambapo usafi wa mazingira katika kituo cha afya kambarage imelenga
kuzuia mazalia ya mbu,na wadudu wengine hatarishi.
Kwa
upande wake kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri BAKWATA Mkoa wa Shinyanga Sheikh
Balilusa Hamis amesema usafi wa mazingira ni sehemu ya ibada katika mafundisho ya dini ya
kiislamu,hivyo amewaomba waumini
kuyaishi mafundisho hayo
Katika
shukrani zake kwa BAKWATA Mkoa wa Shinyanga Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya
kambarage Dkt Ernest Magula amesema usafi uliofanywa na waumini hao ni sehemu ya juhudi za wadau kuzuia mlipuko wa
magonjwa
Jovina
Theodol ametoa shukrani kwa waumini hao kwa zawadi mbalimbali walizowapatia
wagonjwa hao ikiwemo dua.
Sheikh
wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akikabidhi
msaada wa Sabuni na fedha kwa Mama waliojifungua katika kituo cha Afya
Kambarage mjini Shinyanga.
Post a Comment