

Katika kuazimisha siku ya familia ya Polisi Mkoa wa Shinyanga michezo imekuwa chachu ya kunogesha sherehe hizo zilizofanyika Februari 03, 2024 katika Viwanja vya Polisi Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Michezo iliyofanyika ni mpira wa miguu ambapo timu ya Polisi Kahama ilicheza za Polisi Shinyanga kikosi cha tuliza Ghasia na Polisi Kahama kupata ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4.
Pia michezo mingine ilikuwa ni kuvuta kamba, kucheza Ngoma, nyimbo za hamasa pamoja na maonyesho ya jadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi alitoa zawadi kwa washindi mbalimbali, Pia alitoa wito kwa washiriki wote wa michezo kutoishia hapo bali uwe mwendelezo.


Post a Comment