" RC MNDEME AWAKABIDHI ZAWADI ASKARI 10 WALIOFANYA VIZURI ZAIDI SHINYANGA

RC MNDEME AWAKABIDHI ZAWADI ASKARI 10 WALIOFANYA VIZURI ZAIDI SHINYANGA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa zawadi kwa Askari waliotoa huduma bora zaidi kwa wananchi katika kipindi cha mwaka 2023.

Zawadi pamoja na vyeti vya pongezi kwa Askari hao vimekabidhiwa na mgeni rasmi wa sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Christina Mndeme siku ya familia ya Polisi Februari 03, 2024 katika Viwanja vya Polisi Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Polisi - ACP Janeth Magomi alisema kuwa "Jeshi la Polisi litaendelea kuwapongeza Askari watakaokuwa wanafanya vizuri zaidi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kubaini uhalifu na wahalifu"

Pia alitoa wito kwa Askari wengine kuiga mfano mzuri kutoka kwa Askari waliopata vyeti vya sifa katika utendaji wao wa kazi ili kuendelea kutoa huduma bora.

Toka Dawati la Habari Polisi Manispaa ya  Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post