TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Misalaba Media inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kuomba nafasi ya kazi ifuatayo:
VIDEOGRAPHER + GRAPHIC DESIGNER (NAFASI 1)
Sifa za Mwombaji
- Awe na elimu ya Graphic Design au taaluma nyingine zinazofanana.
- Awe na uwezo wa kupiga picha na kurekodi video zenye ubora.
- Awe na uzoefu wa kuhariri video kwa kutumia programu kama Adobe Premiere Pro au nyingine zinazofanana.
- Awe na uwezo wa kutengeneza mabango (posters), thumbnails, logos na kazi nyingine za Graphic Design kwa kutumia Adobe Photoshop au programu zinazofanana.
- Awe mbunifu na mwenye nidhamu.
- Awe tayari kufanya kazi ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga pale inapohitajika.
- Uzoefu wa kufanya kazi kwenye taasisi ya habari au kampuni ya uzalishaji wa maudhui utakuwa ni faida ya ziada.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji watume barua ya maombi pamoja na:
- Wasifu binafsi (CV).
- Nakala za vyeti vya taaluma.
- Sampuli za kazi (Portfolio) au viungo vya kazi walizowahi kufanya (ikiwa vipo).
Maombi yote yatumwe kupitia barua pepe:
misalabamedia@gmail.com
Ofisi Kuu za Misalaba Media zipo Shinyanga Mjini, karibu na Stand ya Zamani.
Mawasiliano
Simu: +255 745 594 231
Mwisho wa Kutuma Maombi
Tarehe 30 Julai, 2026.

Post a Comment