YANGA SC imetinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1 baada ya ushindi wa leo wa mabao 4-1 dhidi ya CFFA katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mabao kwenye mchezo yamefungwa na Ibrahim Kazimoto dakika ya 27 kwa pasi ya Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu amefunga mabao mawili dakika ya 48 na 52, bao la 4 limefungwa na Chuga dakika ya 83.
Bao la CFFA FC limefungwa na Fitahianstoa Albertini dakika ya 74 kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 iliyomshinda Aboutwalib Mshery.
Kikosi cha Yanga SC leo Oktoba 21,2026 kilianza namna hii:Aboutwalib Mshery, Ibrahim Kazimoto, Boka, Komara, Bakari Nondo,Ngoma, Mudathir Yahya, SureBoy, Toure, Seleman Mwalimu na Albert Kangwanda.
Kwenye eneo la wachezaji wa akiba ni Masalangwa, Job, Hussein, Mussa, Maxi Nzengeli, Abushiri, Zakouani, Aziz Ki na Mzize.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment