
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Mndeme Februari 03, 2024 ameungana na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na Familia zao Mkoani humo katika kusheherekea siku ya Polisi (Polisi family day) iliyofanyika katika Viwanja vya Polisi Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Mhe. Mdeme aliwataka Askari wazingatie kauli mbiu ya Jeshi la Polisi ambayo ni nidhamu,haki,weledi na uadilifu, pia amewataka kufanya upelelezi wa kesi kwa haraka ili kupunguza mrundikano wa kesi Mahakamani.
Lakini pia, aliwasisitiza askari kuendelea kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kutojihusisha na uhalifu pamoja na wahalifu
Sambamba na hilo Mhe. Mdeme alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kufichua uhalifu na wahalifu.
Toka Dawati la Habari Polisi Manispaa ya Shinyanga
Post a Comment