Moshi Ndugulile na Mapuli Misalaba
Jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na
wananchi wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, wanaendelea na zoezi la uokoaji kumtafuta
mtoto Salum Mathew aliyesombwa na mto Mhumbu wakati akiogelea.
Mkuu wa jeshi la zimamoto na Uokoaji wa Wilaya ya Shinyanga, Inspekta
Stanley Luhwago anaongoza timu ya askari wa uokoaji inayojumuisha Askari
wa kuogelea na kuzamia pamoja na wananchi.
Amesema zoezi la uokozi limeanza tangu jana majira ya saa moja usiku
lakini lilisitishwa kutokana na mazingira ya giza na kwamba shughuli hiyo
imeendelea tena leo.
Inspekta Luhwago amesema pamoja na juhudi mbalimbali zinazoendelea
kufanyika lakini nguvu kubwa ya maji ni changamoto katika shughuli hiyo ya kumtafuta mtoto huyo.
“Haya maji siyo kwamba yametuama sehemu moja
haya maji yanatembea na yananguvu na katika kutembea inamaana huu mto kutokana
na mvua kubwa iliyonyesha mto umeongezeka upana lakini kuna sehemu tunakutana
na magogo yaliyosombwa na mto kuna mashimo lakini tunaendelea kupambana kwa
kuzingatia usalama”.amesema Inspekta Luhwago
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli Bwana Japhet
Kisusi ameeleza namna alivyopata taarifa na kwamba mpaka sasa shughuli ya
kumtafuta mtoto kwenye mto Mhumbu inaendelea.
“Huyu kijana inasemekana maji yamemchukua
tangu jana jioni saa kumi na moja wakiwa kwenye zoezi la kuvua Samaki walikuwa
wengi kutoka huko Ngokolo wenzake walipojitupia nay eye akafuata mkumbo
alipojitupia basi ndiyo akasombwa na maji”.ameeleza Kisusi
Mjomba wa mtoto aliyesombwa na maji ya mto Mhumbu Bwana Abdallah Sube amesema alipata taarifa hizo jana jioni akiwa
kwenye shughuli zake za utafutaji ambapo ameshukuru na kupongeza juhudi za
jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na wananchi wa Ndembezi katika
juhudi za kumtafuta mtoto huyo.
Watoto waliokuwa wamefuatana na Salumu Mathew wamesema baada ya kuvua
Samaki walianza kuogelea na ndipo mmoja wao alibaini kuwa maji yameanza
kuongezeka lakini wakati wakijaribu kujiokoa ilishindikana Salum alisombwa na maji hayo.
Salum
Mathew mwenye umri wa Miaka 12 ni mkazi wa mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndembezi
katika Manispaa ya Shinyanga anayesoma darasa la Nne Shule ya Msingi Bugoyi B,
Manispaa ya Shinyanga.
Post a Comment