Na Mapuli Kitina Misalaba
Chuo cha Madini Shinyanga (Earth Sciences Institute of
Shinyanga) kimepokea ugeni kutoka THE BRIGHT INSTITUTE, taasisi ya utafiti na
uzalishaji wa betri kupitia madini muhimu ya kimkakati iliyo chini ya Chuo
Kikuu cha North Carolina nchini Marekani, kwa lengo la kujadili na kuona
uwezekano wa kuanzisha ushirikiano wa maendeleo ya teknolojia, utafiti na
mafunzo kuhusu madini muhimu ya kimkakati (Critical Minerals).
Ugeni huo umepokelewa na uongozi wa chuo ukiongozwa na
Mkuu wa Chuo pamoja na Mkurugenzi wa Chuo, ambapo pande hizo zilifanya
mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha Tanzania kunufaika
zaidi na rasilimali zake za madini muhimu ya kimkakati.
Mkuu wa Chuo cha madini Shinyanga, Karebo Peter amesema
ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuiwezesha Tanzania kujenga uwezo wa
kitaalamu katika sekta ya madini muhimu ya kimkakati, ambayo yanahitajika
duniani kwa ajili ya utengenezaji wa betri zinazotumika kwenye magari ya umeme,
mifumo ya nishati ya jua, simu, saa pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumia
betri.
Amesema kupitia ushirikiano huo, chuo kinatarajia
kuongeza uwezo wa kufundisha na kufanya tafiti za kisasa zitakazowezesha
kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kushiriki katika mnyororo mzima wa thamani
wa madini hayo, kuanzia utafiti, uchimbaji, uchakataji hadi utengenezaji wa
bidhaa zenye thamani kubwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chuo hicho Prof.
Athanas Macheyeki amesema ushirikiano huo unatarajiwa kuleta manufaa makubwa
kwa taifa kwa kusaidia kuanzishwa kwa maabara za kisasa za mafunzo na utafiti,
pamoja na kuvutia wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza betri nchini.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itaongeza thamani ya madini
yanayopatikana kwa wingi nchini Tanzania, kuongeza ajira kwa vijana na
kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya The Bright institute Prof.
Hemali Rathnayake amesema taasisi hiyo imevutiwa na fursa zilizopo Tanzania
katika madini muhimu ya kimkakati na inaona umuhimu wa kushirikiana na taasisi
za elimu na utafiti ili kujenga kizazi cha wataalamu kitakachoweza kuongoza
maendeleo ya teknolojia hiyo barani Afrika.
Amebainisha kuwa ushirikiano kati ya taasisi za elimu,
serikali na sekta binafsi ni msingi muhimu katika kuhakikisha rasilimali za
madini zinawanufaisha wananchi kupitia uongezaji thamani na maendeleo ya
teknolojia.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Madini Shinyanga wameeleza
kufurahishwa na ujio wa wageni hao, wakisema umewapa matumaini ya kupata
maarifa mapya, mafunzo ya kisasa, pamoja na fursa za kufanya tafiti na
kushiriki katika miradi ya kimataifa itakayowaongezea ushindani katika soko la
ajira.
Prof. Hemali ameeleza kuwa pamoja na kutembelea Chuo cha Madini Shinyanga, pia imefanya ziara katika taasisi mbalimbali zinazohusika na sekta ya madini nchini, zikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia Tanzania (GST), Wizara ya Madini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ushirikiano wa pamoja katika maendeleo ya teknolojia ya madini muhimu ya kimkakati.
Baadhi ya madini muhimu ya kimkakati yanayopatikana
nchini Tanzania na yenye umuhimu mkubwa katika teknolojia ya kisasa ni pamoja
na Lithium, Cobalt, Graphite, Nickel, Rare Earth Elements (REEs), Tantalum,
Niobium na Manganese, ambayo yanatumika katika utengenezaji wa betri za magari
ya umeme, vifaa vya kielektroniki na mifumo ya nishati safi.
Wakati huo huo, uongozi wa Chuo cha Madini Shinyanga
umewakaribisha vijana na wahitimu wa elimu ya sekondari na vyuo mbalimbali
kujiunga na chuo hicho ili kupata taaluma zinazohitajika katika sekta ya madini
na teknolojia za kisasa.
Uongozi huo umeeleza kuwa chuo kinaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia, maabara na ushirikiano wa kimataifa ili kuwaandaa wataalamu watakaoshiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya madini nchini na duniani.
Mazungumzo ya viongozi wa Chuo cha Madini Shinyanga na wageni kutoka BRIGHT Institute yakijadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya madini na maendeleo ya teknolojia nchini.
Mazungumzo ya viongozi wa Chuo cha Madini Shinyanga na wageni kutoka BRIGHT Institute yakijadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya madini na maendeleo ya teknolojia nchini.
Mkuu wa Chuo cha Madini Shinyanga pamoja na Mkurugenzi wa Chuo wakifanya mazungumzo na ujumbe kutoka BRIGHT Institute ya Marekani kuhusu fursa za ushirikiano katika utafiti, teknolojia na maendeleo ya Madini Muhimu ya Kimkakati.
Mkuu wa Chuo cha Madini Shinyanga, Karebo Peter, akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya chuo katika kuendeleza utafiti, ubunifu na maendeleo ya Madini Muhimu ya Kimkakati kupitia ushirikiano wa kimataifa.
Mkuu wa Chuo cha Madini Shinyanga, Karebo Peter, akitoa wasilisho mbele ya wageni kutoka BRIGHT Institute, akieleza dhamira ya chuo katika kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kukidhi mahitaji ya sekta ya madini nchini na kimataifa.
Mkuu wa Chuo cha Madini Shinyanga, Karebo Peter, akiwasilisha mafanikio, fursa na dira ya chuo katika kuimarisha elimu ya madini na teknolojia kupitia ushirikiano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Chuo cha Madini Shinyanga Prof. Athanas Macheyeki
akiwasilisha mada kuhusu dira ya chuo katika kuimarisha elimu, utafiti na ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo ya Madini Muhimu ya Kimkakati.
Mkurugenzi wa Chuo cha Madini Shinyanga akiwasilisha mipango ya chuo ya kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kuimarisha elimu na teknolojia ya madini.
Wanafunzi na wahadhiri wa Chuo cha Madini Shinyanga wakifuatilia kwa makini mawasilisho kuhusu fursa zinazotokana na Madini Muhimu ya Kimkakati.
Wanafunzi wa Chuo cha Madini Shinyanga wakipata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi kuhusu teknolojia za kisasa za madini.

Wataalamu kutoka BRIGHT Institute wakitembelea maonesho ya sampuli za madini na vifaa vya kisasa vinavyotumika katika mafunzo na utafiti chuoni.

Viongozi wa Chuo cha Madini Shinyanga, wageni kutoka BRIGHT Institute na wakufunzi wakipiga picha ya pamoja baada ya kukamilika kwa ziara iliyolenga kujadili ushirikiano katika maendeleo ya Madini Muhimu ya Kimkakati na teknolojia zake.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment