Mahakama kuu kanda ya Shinyanga chini ya uongozi wa Jaji mfawidhi wa Mahakama hiyo Frank Habibu Mahimbali, imetoa cheti cha pongeza kwa taasisi ya Misalaba Media, kwa kuripoti habari za Mahakama kwa weledi hasa kipindi cha maadhimisho ya wiki ya sheria Nchini.Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi Januari 24 ambapo kilele chake kimefikia Februari Mosi mwaka huu 2024 na kwamba kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa: nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi kwa haki jinai”.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme upande wa kulia akimkabidhi cheti cha pongezi na shukurani Mkurugenzi wa Misalaba Media, Mapuli Kitina Misalaba kwa kuripoti habari za Mahakama kwa weledi hasa kipindi cha maadhimishi ya wiki ya sheria Nchini.
Cheti cha Misalaba Media.MISALABA MEDIA tunajihusisha na Utafutaji, uandaaji na usambazaji wa habari mtandaoni ikiwemo habari za Siasa, sherehe na habari za matukio mbalimbali ikiwemo ukatili.Endelea kutembelea mitandao yetu kila wakati, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba ya Simu 0745594231 Au tuma habari yako kwenye email: misalabablog1@gmail.com


Post a Comment