Na Mapuli Kitina Misalaba
Wakazi wa mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya
Shinyanga wamewaomba wakala wa Barabara mijini na vijijini
TARURA Mkoa wa Shinyanga kukarabati daraja lililopo karibu na
makaburi eneo la Dodoma ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Wakizungumza na Misalaba Media wamesema kutokana na Mvua
zinazoendelea kunyesha Maji yamekuwa yakijaa na kulifunika daraja
hilo hali ambayo husababisha watoto hasa wanafunzi kushindwa kuvuka
Wamesema daraja hilo linahatarisha usalama wao hasa kipindi cha Mvua
ambapo wameiomba serikali kupitia TARURA Mkoa wa Shinyanga
kuchukua hatua za haraka kukarabati daraja hilo ili kuepusha usumbufu
uliopo.
Elizabeth Richard ni mkazi wa mtaa wa Butengwa ameeleza
changamoto wanayokutana nayo wakati wa kuvuka mto unaounganisha
eneo la Mageuzi na Dodoma kata ya Ndembezi.
"Muda ukifika wa wanafunzi kutoka shule kama mvua imenyesha tunawafuata ili kuwavusha maana hawawezi kupita wao wenyewe tu mfano leo wanafunzi hawajaenda shule maji yalikuwa ni mengi maji haya huwa yanaingia mpaka kwenye nyumba zetu mfano mimi yalijaa mpaka ndani kwangu kwa kweli tunaona kabisa yanatuletea athari tulikuwa tunaomba tuletewe daraja haya maji bila daraja yatatuathiri sana".amesema Elizabeth
Post a Comment