Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA BINTI MSAFI FOUNDATION LATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE ZAIDI YA WANAFUNZI 185 SHULE YA SEKONDARI LYASIKIKA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Shirika lisilo la kiserikali la Binti Msafi Foundation limetoa Taulo za kike kwa Wanafunzi takribani 185 katika shule ya Sekondari Lyasikika kata ya Machame Mashariki Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Irene lema amesema shirika hilo litaendelea kuwasaidia Wanafunzi wa kike katika Wilaya hiyo kwa kuwa wanafunzi wengi hushindwa kujistili wakati wa masomo na kipindi cha mitihani.

"leo tumekabidhi Taulo za kike kwa wanafunzi zaidi ya 185 huu ni atamaduni wa shirika hili  kusaidia Wanafunzi wa kike katika Wilaya  ya Hai kutona na Wanafunzi wengi kushindwa kujistili wakati wa masomo na kipindi cha mitihani".amesema Mkurugenzi Irene

Mkurugenzi huyo wa shirika la Binti Msafi Foundation Bi. Irene Lema ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa watanzania kuona umuhimu wa kusaidia watoto wa kike katika Wilaya zenye changamoto hiyo ili waweze kusoma na kuhitimu salama masomo hayo.

Amesema  Shirika litaendelea kutoa msaaada kwenye maeneo mengine na kusaidia katika utunzaji wa mazingira ili kuirejesha kilimajaro ya zamani yeye uoto wa asili mzuri kwa kuongeza  jitihada za upandaji wa miti kwa kila taasisi binafsi na za umma.

Sambamba na zoezi hilo shirika  limeotesha Miti kwa ajili ya Kutunza na kubotesha mazingira shuleni hapo

Kwa upande wake Eng Pamela Massay, naye amesisitiza wananchi kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira kayika Mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla ili kukabiriana na tabia nchi.

Mkurugenzi wa shirika la Binti Msafi Foundation Bi. Irene lema akiwa amebeba boksi la Taulo za kike.



Post a Comment

0 Comments