HomeHABARI SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YATOA ELIMU YA UKATILI KWA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI LITTLE TREASURE Misalaba February 16, 2024 0 Uongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, siku ya leo Ijumaa Februari 16,2024 umetoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili katika shule ya secondary Little treasure, iliyopo Manispaa ya Shinyanga. Viongozi hao ni pamoja na katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya, Mwenyekiti wa Michezo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Inspekta Alkwin Willa, katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Husna Maige na mjumbe idara ya maafa uhitaji na makundi maalum Vedastina Nyankonga. Viongozi hao wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wameambatana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo afisa kutoka dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Shinyanga mjini Jane Mwasembe pamoja na afisa maendeleo ya jamii wa kata Neema Kalinga.Viongozi hao wamewataka wanafunzi kuepukana na mazingira hatarishi yanayoweza kupelekea ukatili ikiwemo kubakwa kwa wanafunzi wa kike.Wamewasisitiza kutoa taarifa za viashiria vya ukatili kwa walimu wao, viongozi wa serikali au kupiga simu namba ya bure 116 ili kuepukana na athari zitokanazo na ukatili ambazo zinaweza kukwamisha ndoto zao.Aidha wanafunzi wa shule hiyo wamefurahi na kupongeza kwa elimu hiyo ambayo huku wakiahidi kuwa kielelezo katika masuala ya kupambana na ukatili kwa lengo la kuimarisha usalama wao.Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya aliyesimama upande wa kushoto akitoa elimu ya ukatili katika shule hiyo.Picha ya pamoja.Mwenyekiti idara ya Michezo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Inpekta Alkwin Willa akitoa elimu kuhusiana na umuhimu wa Michezo katika kuepukana na vitendo vya ukatili hasa kwa wanafunzi. You Might Like View all
Post a Comment