Wakazi wa vijiji vitatu katika kata ya chifunfu wilayani Sengerema mkoani Mwanza wailalamikia Wakala wa maji vijijini ( RUWASA ) kwa kutowapatia huduma ya mradi wa maji safi ambao umetekelezwa katika kata hiyo na kupelekea kutumia maji yasiyokuwa safi na salama kutoka katika mito na kusababisha kutokea kwa ugonjwa wa kipindupindu hivi karibuni.
Kero hiyo wameitoa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasam ambapo wamesema kumekuwa na hujuma kadhaa za kutakiwa kupatiwa huduma hiyo muhimu huku wakitakiwa kununua baadhi ya vifaa vya kusambaziwa mahitaji hayo kwa gharama kubwa kitendo kilichowafa wao kukukosa huduma hiyo muhimu ya kibinadamu.
Mradi huo ambao umetekelezwa kwa zaidi ya shilingi bilioni mbili ambao ulianza kutekelezwa tangu February mwaka 2022 na unatajwa kukamilika mwaka huu lakini wakala hiyo umeshindwa kuwapatia wakazi hao huduma hiyo.
Akijibu tuhuma hizo kaimu Meneja wa Wakala hiyo Magembe Makalanga amesema kwasasa mradi huo upo kwenye majaribio hivyo huku akisema kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu zoezi la kuwaunganishia wateja maji majumbani litaanza.
" Mradi huu utahudumia kata ya Chifunfu yenye vijiji vitatu ambayo ni, Chifunfu,Lukumbi na Nyakahako ambao unatarajiwa kuhudumia watu zaidi ya elfu 31 huku wateja wetu mia 200 wataipata huduma hiyo bure,"Magembe Makalanga - Kaimu Ruwasa Sengerema "
Kufuatia hali hiyo Mbunge wa Jimbo hilo Hamis Tabasam ametoa siku 21 kwa Wakala hiyo kuhakikisha wakazi zaidi ya mia nane ambao tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupata huduma hiyo wakiipata.
"Muweke utaaratibu wa kuwapa uhuru wananchi kumudu kununua vifaa vya kuunganishiwa huduma ya maji ambavyo wao wataweza kuvinunua kwa gharama nafuu na vilivyo bora na vyenye kudumu muda mrefu kuliko kuwapatia masharti ambayo yatapelekea wao kushindwa kuvimudu hivyo nawapa siku 21 kuanzia leo wananchi waweze kupata huduma ya maji,Hamis Tabasam - Mbunge wa Jimbo la Sengerema"
Nao baadhi ya wananchi mradi huo umetekelezwa katika maeneo yao na wale ambao waliopitiwa na mradi na wengine kutoa mashamba wakailalamikia Wakala hiyo kwa kutowapatia kipaumbele kwa ajili ya kunufaika na mradi wa maji hayo wakamuomba Mbunge wao piya waweze kupewa kipaumbele cha kuweza kuipata huduma hiyo kutokana na wao kutohusishwa na mradi huo wa maji safi na salama.


Post a Comment