" PAUL CHACHA AANZA KAZI TABORA, AAHIDI KUSIMAMIA HAKI MAENDELEO NA USALAMA

PAUL CHACHA AANZA KAZI TABORA, AAHIDI KUSIMAMIA HAKI MAENDELEO NA USALAMA

 Na Lucas Raphael - Misalaba Media,Tabora 

Mkuu mpya wa mkoa wa Tabora Paul  Chacha amesema kwamba amekuja tabora kwa ajili ya  kusimamia haki, usalama na maendeleo ya wananchi wa mkoa wa  huo.

Kauli hiyo alitoa Machi 18,2024 alipokuwa akizungumza katika kikao cha  pamoja na watumishi wa kanda mbalimbali za mkoa huo wakati   kukaribishwa wake kwenye ukumbi wa mtemi Isike Mwanakiyungi  

 

Chacha alisema kwamba moja ya vipaumbele vyake ni Haki ,usalama na maendeleo,pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi hivyo kila kiongozi kuhakikisha anasimama eneo lake la kiutawala na wasaidia wananchi kuvuka hapa tulipo.

 

Aidha  ajitambulisha kuwa yeye ni  mtu mwenye msimamo, muumini wa haki na kuahidi kwamba katika kusimamia haki na maendeleo ya mkoa wa Tabora Kwa kushirikiana na viongozi na wananchi wa halmashauri zote za mkoa huo.

Hata hivyo alifafanua kwamba kuna  kesi ya mauaji ambayo aliiacha miaka miwili iliyopita alipokua mkuu wa wilaya ya Kaliua ambapo mwanaume mmoja alituhumiwa kuwaua watoto wawili wa mke wake na kuwazika ndani kisha kutokomea kusikojulikana na kuliagiza jeshi la polisi kumsaka na kumkamata mtuhumiwa huyo.

Alisisitiza kwamba vitendo vya ukali kwa wanawake na watoto  hatoweza kuvifumbia macho katika kipindi ambacho hatakuwa mkoani hapa hatopenda viendelee kujitokeza na kuwaomba viongozi  wa dini kuhakikisha wanakemea vitendo vyote viovu.

 
Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya aliahidi ushirikiano Kwa niaba ya watumishi wengine wa mkoa huo.

Alisema kwamba mkoa una watumishi waadilifu na wachapa kazi ambao watamsaidia kutimiza majukumu yake mapya kama mkuu wa mkoa.

Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Ramadhani Kapela alishukuru kwa niaba ya wenyeviti wa halmashauri za mkoa wa Tabora na  kusema ni matumaini ya wengi kwamba atautumikia mkoa wa Tabora kwa ufanisi kwakua yeye si mgeni katika mkoa huo.

Mkuu wa mkoa mpya Paul Matiko Chacha anachukua nafasi ya aliyekua mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian aliyehamishiwa mkoani Tanga katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu siku chache zilizopita.

Post a Comment

Previous Post Next Post