Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Bunda Mara
Silas Samson mkulima wa zao la pamba katika mtaa wa Kuzungu wilayani Bunda mkoani Mara ameishauri Serikali pamoja na Bodi ya Pamba nchini kuhamisha wakulima wa zao hilo kuanza kulima kilimo hicho ifikapo mwezi Septema kila mwaka ili kuondokana na changamoto ya wadudu akiwemo chawa jani.
Afisa kilimo wa kata ya Kuzungu Juma Thomas Malima amesema,awali kilimo katika kata hiyo kimekuwa kikifanyika mwezi Novemba na msimu uliopita kilimo cha zao la pamba kimefanyika mwezi Septemba na matokeo yake yamekuwa mazuri likiwemo shamba la Silas Samson ambaye alipanda mwezi Septemba huku akisema pamba ya mwezi wa Septemba imefanya vizuri kuli ya mwezi Oktoba.
" Tuna tatizo la chawajani tunapolima pamba ya mwezi wa tisa sehemu kubwa inakuwa inasaidia yaani mpaka mashambulizi ya chawajani yaje kuanza mwezi Machi unakuta tayari umevuna pamba kwa kiasi kikubwa,"Juma Thomas Malima - Afisa kilimo wa kata ya Kuzungu.
Naye Mtendaji wa kata hiyo Lusasu Mhando akizungumza na Jambo Digital amesema, zipo changamoto kadhaa kwa misimu iliyopita kwa wakulima waliopanda miezi ya Oktoba,Desemba na January awakuweza kupata mazao mengi hata hivyo ameongeza kuwa , msimu wa mwaka 2023/2024 wamewahamasisha wakulima waweze kulima mwezi Septemba ambao umeonekana kuwa bora zaidi kuliko miezi mingine ya uzalishaji na kutoa mavuno mengi kwa hekali moja kilo mia nanena hivyo kumuongezea mkulima kipato zaidi.
Post a Comment