Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Victor Mkwizu, leo Julai 31, 2025 amekabidhiwa rasmi barua ya uteuzi wa kushiriki katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatua inayompa nafasi ya kuwania tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025.
Akizungumza na Misalaba Media baada ya kukabidhiwa barua hiyo, Mkwizu amesema ana dhamira thabiti ya kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kati ya mwaka 2021 hadi 2025 katika kata hiyo, akibainisha kuwa kata ya Ngokolo imekuwa miongoni mwa kata zilizofanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Tumefanikisha mambo mengi, hasa kwenye sekta ya miundombinu ya barabara, huduma za kijamii na utatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi. Ninaomba ridhaa ya wana Ngokolo ili tuendelee na safari hii ya maendeleo kwa kasi zaidi,” amesema Mkwizu.
Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, wagombea wote waliopitishwa wanatarajiwa kushiriki katika kura za maoni ndani ya chama hicho hivi karibuni ili kupata wagombea watakaowakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Post a Comment