" UWT WILAYA YA SHINYANGA MJINI WAFANYA KONGAMANO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

UWT WILAYA YA SHINYANGA MJINI WAFANYA KONGAMANO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Moshi Ndugulile na Mapuli Kitina Misalaba

Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini leo wamefanya kongamano lililojumuisha takribani wanawake 400,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 12,2024 katika ukumbi wa mikutano wa CCM  Mkoa wa Shinyanga, ambapo limejumuisha uwakilishi wa wanawake kutoka makundi mbalimbali wakiwemo wastaafu, viongozi wa taasisi na asasi za kiraia,  wajane, wajasiliamali, wenye ulemavu,na viongozi wa wanawake wa jumuiya zote za chama cha Mapinduzi CCM ngazi ya tawi, kata hadi Mkoa.

Katika kongamano hilo zimewasilishwa mada mbalimbali ikiwemo mwanamke na uongozi,ujasiliamali,ukatili wa kijinsia pamoja na mada inayohusu maadili na ndoa.

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi, katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo amesema mmomonyoko wa maadili unatokana na Ndoa zenye migogoro isiyokwisha hivyo amewataka Wanawake kusimama imara katika jukumu la kuwajibikia nafasi yao kama Mama na viongozi katika ngazi ya familia na jamii.

Ametoa wito kwa Wanawake kuwa na umoja na mshikamano na kupaza sauti za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto.

Amezungumzia pia uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye Mwaka huu na uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwaka kesho 2025 kwamba Wanawake wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewaomba Wanawake kuendeleza umoja na mshikamano ili kusukuma maendeleo mbele.

Nhemanilo amewaomba Wanawake kuendelea kuiunga mkono serikali katika juhudi na hatua za kufikia mafanikio.

Akizungumza katika kongamano hilo katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) amewataka Wanawake wa Wilaya ya Shinyanga kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika badaye Mwaka huu 2024 na uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwaka kesho 2025 ili kuleta uwiano baina yao na wanaume katika nafasi za uongozi.

Amesema ili kwenda sanjari na kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mwaka huu 2024 inayosema wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii, Wanawake wanapaswa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ili kuweka uwiano sawa wa Wanaume na Wanawake katika uongozi.

Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Msanii Richard Masele amesema chama hicho kinatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo na ustawi wa Nchi.

Naye naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban ameeleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na serikali kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni msukumo na usimamizi mzuri wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaofanywa na wabunge pamoja na madiwani.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akizungumza katika kongamano hilo.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akizungumza katika kongamano hilo.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema Nhamanilo akizungumza katika kongamano hilo.


Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema Nhamanilo akizungumza katika kongamano hilo.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) akizungumza kwenye kongamano hilo.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) akizungumza kwenye kongamano hilo.

Katibu wa itikadi, siasa na uenezi  wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Msanii Richard Masele akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Wanawake wakiendelea na Burudani kwenye kongamano hilo.












 

Post a Comment

Previous Post Next Post