" MWANAMKE MCHAGA ANAYEFANYA MAAJABU KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KAGERA

MWANAMKE MCHAGA ANAYEFANYA MAAJABU KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KAGERA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MissenyiBi. Neema Martin Mushi, ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, ni mfano bora wa ujasiri na ubunifu wa wanawake wa Kiafrika. Akiwa na matumaini na malengo makubwa, Bi. Mushi anaukabili ulimwengu wa ufugaji wa Nguruwe, kuku, sungura, na bata kupitia mradi wake unaojulikana kama NEY PIG FARM, uliopo wilayani Missenyi, Mkoa wa Kagera.Katika kazi yake ya kila siku, Bi. Mushi pia anahusika na ufundishaji kama mwalimu katika Shule ya Sekondari Kasambya. Alianza kazi hiyo mwaka 2015, lakini aligundua kuwa ufugaji unaweza kuwa njia nzuri ya kuongeza kipato na kuboresha maisha yake na ya wengine katika jamii yake. Lengo lake ni kufikia ufugaji wa nguruwe 500, alianza na nguruwe mmoja pekee aliyemwezesha kujenga mafanikio ya ajabu akiwa na zaidi ya nguruwe mia moja hivi sasa.Bi. Mushi ameeleza jinsi alivyovutiwa na mazingira ya Missenyi, ambayo yanarudisha kumbukumbu za nyumbani kwao Moshi. Aliamua kuleta mabadiliko katika eneo hilo, si tu kwa ajili yake, bali pia kwa jamii kwa ujumla. Akiwa na ufugaji huo, ameruhusu vijana wa eneo hilo kupata ajira na kujenga maisha bora, ambapo anatumia sehemu ya faida yake kuwasaidia majirani, akijumuisha kutoa nguruwe jike na mbolea bure.Katika mahojiano yake, Bi. Mushi anasisitiza umuhimu wa wanawake kujitokeza katika shughuli za kiuchumi, akiwashauri wasiogope kuchukua hatua na kujihusisha na ufugaji. Amepongeza ushirikiano alioupata kutoka kwa maafisa wa kilimo wa Wilaya ya Missenyi na jamii yake, ambayo imemsaidia kufanikiwa.Amesema kuwa kuwa cha ya changamoto zinazohusiana na ufugaji, kama vile kuwapatia chakula na kuwatibu nguruwe, anajisikia fahari kutoa mchango wake kwa jamii. Pia amewashukuru wateja wake na wanafamilia wanaotambua mchango wa shughuli zake anazoendesha.Bi. Mushi anatumia mifano ya mafanikio yake kuwahamasisha wanawake wengine wajituke na kujiingiza katika ufugaji na biashara za kilimo kwani unachangia kuondoa umaskini na kuleta maendeleo.hata hivyo Bi. Mushi amewaomba wateja wake kumfikia kwani anafanya biashara hiyo kwa kuuza nguruwe wa mwezi mmoja, aliyezaa, mwenye mimba, hadi vitoto.

Post a Comment

Previous Post Next Post