Na Mapuli Kitina Misalaba
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga
(SHUWASA) imeungana na taasisi nyingine za serikali na wadau mbalimbali
kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika
Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza Machi 8, 2026 wakati wa maadhimisho hayo, Angel
Mwaipopo, kutoka SHUWASA amesema mamlaka hiyo inaendelea kushirikiana na
serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa
urahisi, huku wanawake na wasichana wakiwa miongoni mwa wanufaika wakubwa wa
huduma hiyo muhimu.
Amesema upatikanaji wa maji kwa muda wote ni hatua
muhimu ya kupunguza mzigo kwa wanawake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakibeba
jukumu kubwa la kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya familia, hali inayowapa
nafasi zaidi ya kushiriki katika shughuli za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
“SHUWASA inaendelea kuboresha miundombinu
ya maji na kusogeza huduma karibu na wananchi ili wanawake na wasichana
wasitumie muda mwingi kutafuta maji, badala yake waweze kujikita katika elimu,
biashara na shughuli nyingine za maendeleo,” amesema Mwaipopo.
Maadhimisho hayo yamefanyika chini ya kauli mbiu
isemayo “Haki kwa Wanawake na Wasichana: Msingi wa Maendeleo Jumuishi Kufikia
Dira ya 2050.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni
Mhita, amesema mwanamke anapaswa kujiona kuwa wa thamani kubwa katika jamii na
kujitambua, kwani namna anavyojichukulia ndivyo jamii itakavyomchukulia.
Amesisitiza kuwa wanawake wanapaswa kuendelea kutumia fursa zinazotolewa na serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji na uchumi ili kuchangia kikamilifu maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment