" WANANCHI WAMEMWOMBA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANAMRINGI MACHA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZILIZOPO

WANANCHI WAMEMWOMBA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANAMRINGI MACHA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZILIZOPO

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamemwomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kushughulikia Changamoto zilizopo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Barabara  wakiitaja Barabara kipande cha kutoka Ndala, kupitia Masekelo  kwenda Mwawaza ilipo Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wananchi hao wamemwomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  kuendelea kutatua kero na changamoto za muda mrefu ikiwemo kuiboresha Barabara hiyo ya kuelekea Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wametoa maoni hayo wakati wakizungumza na Misalaba Media ikiwa ni siku mbili baada ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kukabidhiwa ofisi siku chache baada ya kuapishwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufuatia uteuzi wake uliofanyika March 12,Mwaka huu

Wameshauri pia kuwa itapendeza iwapo Mkuu wa Mkoa atajenga utaratibu wa kusikiliza kero za Wananchi kupitia Mikutano ya hadhara ili kufahamu changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko kuu mjini Shinyanga wameomba kuharakishwa kwa ukamilishaji wa soko kuu la Mjini Shinyanga ambalo wamesema ujenzi wake umekuwa ukisua sua.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post