" ASKOFU MKUU WA AICT MAGWESELA AWATAKA WAZAZI KUENDELEZA KALAMA ZA WATOTO KANISANI

ASKOFU MKUU WA AICT MAGWESELA AWATAKA WAZAZI KUENDELEZA KALAMA ZA WATOTO KANISANI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Askofu Mkuu wa kanisa la AICT Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Mwanza Mussa Magwesela amewataka Wazazi na Walezi kuwa chachu ya kukuza na kuendeleza karama za watoto katika maisha ya kanisa.

Ameyasema hayo leo wakati akihubiri kwenye ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga, ambapo amesema kanisa linatambua na kuthamini  karama  za watoto hivyo kwa kushirikiana na wazazi na walezi, litaendelea  kuibua uwezo wao na kuwaendeleza kupitia vipaji vyao.

Amesema hatua hiyo itasaidia kutimiza ndoto za watoto na kuendelea kulitumikia taifa katika misingi ya Dini.

Askofu huyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakristo kuendelea kuishi maisha ya kumtumikia Mungu kwa utii,unyenyekevu na mapendo zaidi kuanzia ngazi ya familia, kwenye maeneo ya  kazi, Biashara na shughuli mbalimbali za kijamii.Ibada ya Jumapili ikiendelea leo Aprili 7,2024 katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post