" TAASISI YA DINI YA KIISLAM YA THAAQIB YAAHIDI KURUDISHA UFAULU WA DIVISION ONE KWA KIDATO CHA KWANZA NA NNE.

TAASISI YA DINI YA KIISLAM YA THAAQIB YAAHIDI KURUDISHA UFAULU WA DIVISION ONE KWA KIDATO CHA KWANZA NA NNE.

TAASISI ya Dini ya Kiislam ya Thaaqib yenye Makao makuu yake Jijini Mwanza eneo la mtaa wa Ghana   inayomiliki   Nyasaka Islamic sekondari school pamoja na  Thaaqib Islamic preimary school iliyopo eneo la  Kiloleli wamefanya tamasha la usafi  katika shule ya Nyasaka Islamic sekondari schol baada ya miaka 10 kuwa mikononi mwa IPC hata hivyo wameahidi kurudisha UFAULU   wa DIVISIO ONE hapo awali kwa kidato cha KWANZA na kidato cha NNE kama  ilivyokuwa awali huku wakitoa  wito kwa wazazi kupeleka wanafunzi katika shule hizo.

Kiongozi wa Taasisi ya Thaaqib, Alhaj Nurdin Simba amesema,waislam wamefika   Nyasaka Islamic sekondari school kufanya usafi kutokana na uwepo wa uchafu katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo ili wanafunzi watakaporejea kutoka likizo wakute mazingira masafi na salama vikiwemo vyoo pamoja na mabweni.


AMIR  wa Taasisi ya Dini ya Kiisalam ya Thaaqib, Mshumba Alfan Almas  amesema baada ya kukabidhiwa shule ya sekondari ya Nyasaka Islamic wakaona ipo haja ya kuwakusanya waislam ili kuweka mazingira safi  kutokana na wanafunzi kuwa katika mazingira magumu kipindi shule ziko katika Taasisi ya IPC.


Post a Comment

Previous Post Next Post