Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameonya kuhusu tabia ya ubinafsi na kuwataka waumini kuwa chimbuko la huruma ya Mungu kwa maneno na matendo yao, huku wakiyaangalia zaidi makundi yenye uhitaji wakiwemo wajane na watoto yatima.
Askofu Sangu ameyasema hayo wakati akihubiri kwenye adhimisho la Misa takatifu ya Dominika ya Huruma ya Mungu, ambayo imefanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Nkololo Wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambapo ni kituo cha kijimbo cha hija ya huruma ya Mungu.
Amesisitiza waumini na jamii kutafakari zaidi kuhusu madhara ya ubinafsi na kusisitiza kuishi maisha ya kuwahurumia wengine na kuguswa kuwasaidia kadiri ya mahitaji yao kama Mungu alivyo na huruma kwa wanadamu.
Askofu Sangu ameendelea kuwaonya watu wenye tabia ya kutumia shida za wengine kama fursa ya kujinufaisha badala ya kuwasaidia.
Leo Kanisa Katoliki kote ulimwenguni limeadhimisha Dominika ya huruma ya Mungu ambayo huadhimishwa kila Mwaka siku ya jumapili ya pili ya Pasaka, ikiwa ni sehemu ya kufanya tafakari ya kina juu ya huruma ya Mungu kwa wanadamu.
Katika Jimbo Katoliki Shinyanga maadhimisho hayo ambayo hutanguliwa na mafunga pamoja na sala kwa ajili ya nia mbalimbali hufanyika katika kituo cha kijimbo cha hija ya Huruma ya Mungu kilichopo katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Nkololo Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, ambapo hukutanika, Mapadre, watawa na waamini kutoka seghemu mbalimbali za Jimbo.

Bango lililopamba maadhimisho ya Dominika ya huruma ya Mungu katika Parokia ya Nkololo

Wanakwaya wakiwa kwenye maandamano kuingia kanisani kwenye adhimisho la Misa


Askofu Sangu,Mashemasi na Mapadre wakiwa kwenye maandamano kuingia kanisani kwenye adhimisho la Misa ya Dominika ya Huruma ya Mungu


Askofu Sangu akibariki maji kabla ya adhimisho la Misa



Askofu Sangu akiwanyunyuzia maji ya baraka waamini walioshiriki adhimisho la Misa ya Dominika ya Huruma ya Mungu

Msomaji wa somo la kwanza akisoma somo

Msomsji wa somo la pili akisoma somo

Shemasi Paschal Mahalagu akisoma somo la Injili takatifu

Askofu Sangu akitoa mahubiri wakati wa adhimisho la Misa

Waamini wakifuatilia mahubiri kutoka kwa Askofu Sangu


Askofu Sangu akiwaongoza waamini kusali sala ya majitoleo kwa huruma ya Mungu

Askofu Sangu,Mapadre,Mashemasi na Watumikiaji wakitoa heshima kwenye sura ya Yesu kwa kuinama

Paroko wa Parokia ya Nkololo (wa kwanza kulia) Padre Paul Fegan akiwa na Mapadre wakati wa sala maalum kwa heshima ya huruma ya Mungu

Wanakwaya wakiimba wakati wa adhimisho la Misa

Adhimisho la Misa takatifu ikiendelea kanisani



Mapadre wakiwakomunisha waamini





Shemasi Paschal Mahalagu akiwakomunisha watumikiaji

Paroko wa Parokia ya Nkololo Padre Paul Fegan akitoa neno la shukrani kwa Askofu Sangu na waamini baada ya adhimisho la Misa


Askofu Sangu akitoa baraka kwa waamini baada ya adhimisho la Misa
Post a Comment