Na Mary Mosha, SIHA
BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Munge wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro wamesema upatikanaji wa daraja la Upinde wa Mawe litawarahishia mawasiliano katika kijiji na kijiji, kupunguza utoro shuleni pamoja na kupata mahitaji ya msingi kwa urahisi.
Wakizungumza mara baada ya mwenge wa uhuru kuweka jiwe la msingi akiwemo Florah Letaiyo alisema, awali nyakati za mvua walikuwa wakilala njaa kutokana na kukosekana kwa mawasiliano katika eneo hilo.
"Wanafunzi wengi hukosa shule sikumbili hadi sita hasa nyakati za mvua.kama hujanunua mahitaji au kusaga unga mvua zinaponyesha ni ngumu kupata maana upande wa juu ndiko zinakopatikana na hutenganishwa na daraja,"alisema Julieth Molel
Baadhi ya madereva akiwemo Abel Saruni alisema kukamilika kwa daraja hilo kunaweza kukuza Uchumi wa madereva bodaboda, na jamii kwa ujumla.
Naye Diwani wa viti maalumu wa Kata Donyomoro, Lillian John alisema kabla ya daraja hilo wapo baadhi walishasombwa na maji wakielekea kwenye utafutaji wa majukumu.
"Kulikuwa na utoro mwingi shuleni hasa nyakati za mvua hivyo kuwafanya baadhi ya wazazi hasa ya jamii ya wafugali kukata taama,"alisema
Akisoma taarifa Mtendaji wa kijiji hicho, Winner Muro alisema mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya milion 35 zikiwemo fedha za mapato ya ndani ya halimashauri zaidi ya milion 27 wafadhili(TASAF)zaidi ya milion 540 na michango ya jamii zaidi ya milion 7 na kutoa ajira wananchi 13.
Aidha akiweka jiwe la msingi, kiongozi wa mbio za mwenge 2024, Godfrey Mzava aliitaka viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanafanya mawasiliano na wananchi waliopo pembezoni mwa hifadhi ya barabara na kuona namna ya kuwafidia au kupisha ili kuepuka madhara yatokanayo na kuishi pembezoni mwa barabara lilipo daraja hilo.
"Mradi tumeukaugua na kuutembelea, umekamilika kwa asilimia 96 na hii ndogo iliyobaki ni vitu vidogo vidogo, vikamilishwe.Wananchi ni wajibu wenu kuwa walinzi wa miradi hii ili thamani ya fedha ya serikali kuleta tija kwa jamii, "alisema Mzava.
Post a Comment