Na Elisha Petro
Mechi ngumu katika hatua ngumu kwenye michuano migumu zaidi Duniani ngazi ya vilabu, hii ni mechi iliyobeba kisasi ndani yake na utafutaji wa ufalme kwa vijana wa Carlo Ancelotti dhidi ya vijana wa Pep Guardiola hatua ya robo final michuano ya UEFA.
Katika michezo 12 ya mwisho Real Madrid wameshinda michezo minne (michezo mitatu wakiwa nyumbani na mmoja wakiwa ugenini) lakini wamepoteza michezo mitano (minne wakiwa ugenini na mmoja wakiwa nyumbani) na wametoka sare michezo mitatu pekee (michezo 2 Manchester City akiwa nyumbani na mmoja Madrid akiwa nyumbani).
Misimu miwili ya mwisho kwenye UEFA wamekutana hatua ya nusu final kwanza 2021/2022 Madrid alitinga final kwa jumla ya magoli 6-5 baada ya kichapo cha goli 4-3 akiwa ugenini na baadae alishinda akiwa nyumbani goli 3-1 na msimu wa 2021/2023 Manchester City alifanikiwa kumtoa Madrid kwa jumla ya goli 5-1 baada ya sare ya goli 1-1 akiwa ugenini na baadae akiwa nyumbani alishinda goli 4-1 yaani yamefungwa magoli 17 katika michezo minne ya mwisho.
Aina ya uchezaji wa Real Madrid na Manchester City unafanana wote wanacheza na wakiwa na lengo la kushambulia ili kupata goli na kushinda mchezo ndiyo maana kwenye michezo yao 12 ni michezo mitatu pekee ambayo hawakufungana kila mmoja ila michezo tisa mmoja alipata goli na kwa hivi karibuni kwenye michezo mitano ya mwisho ni mechi moja pekee ambayo hawakufungana ila michezo minne Kila mmoja alipata goli.
Mwisho kabisa kunauwezekano wa kila timu kupata goli kwenye mchezo wa leo April 9,2024 kwa aina ya wachezaji kama Vinicius Junior, Jude Bellingham na Rodrygo kwa Madrid lakini hata kwa Manchester City uwepo wa Haaland, Foden kwenye kiwango kizuri sana pamoja na Kelvin De Bruyne mmwenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi zinazoweza kuzaa matunda kwao.
Post a Comment