Na Mapuli Kitina Misalaba
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imetoa warsha kwa
waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwakumbusha kuhusu
wajibu wa kuzingatia miiko na maadili ya
kazi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi.
Akiwasilisha mada kuhusu maana na majukumu ya mamlaka ya
TCRA, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kanda
ya ziwa Mhandisi Imelda Salumu pamoja na mambo mengine amewahimiza waandishi wa habari kuwahamasisha
watanzania kuingia kwenye Uchumi wa kidijitali ili kuendelea kunufaika na fursa
mbalimbali.
Amesema Sekta ya Mawasiliano
imeendelea kukua na kufungua fursa mbalimbali hivyo amewasisitiza waandishi
wa habari kuwahamasisha watanzania kuingia kwenye Uchumi wa kidijitali pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii.
“Tujue kwamba tupo kwenye ulimwengu wa kidijitali na uchumi
wa kidijitali Dunia yote kwa sasa hivi iko huko na kila nchi iko kwenye nafasi
tofauti kulingana na sera, sheria zilizoko kwenye nchi husika sisi pia tuko
huku yaani sisi TCRA tupo kama dereva au kama nahodha tunaendesha hivyo vyombo
mbalimbali vya kuwapeleka watanzania kwenye uchumi wa kidijitali lakini
hatuwezi kufanya hicho kitu peke yetu tunahitaji wadau wote waelewe kwamba hata
mwananchi wa kawaida kama anataka kupata huduma kwa nini ahangaike mara asafiri
atumie nauli yake apoteze muda kufuata huduma sehemu furani tunataka hiyo
huduma aipate mtandaoni tu”.
“Mitandao ya kijamii
imejitokeza na kuendelea kuwa vyombo vya kusambaza habari na taarifa mbalimbali
imerahisisha mawasiliano kwa watumiaji kupata habari kwa wakati ni vyema sasa
waandishi wa habari mkaendelea kujilinda kwa kuepuka kusambaza habari au
taarifa za uongo na uzushi”.amesema Mhandisi Imelda
“Sekta ya mawasiliano
nchini inahusisha miundombinu, utoaji na matumizi ya huduma na bidhaa katika
sekta ndogo za simu na intaneti, utangazaji na post, huduma za mawasiliano ni
za msingi katika maisha ya wananchi kijamii, kiuchumi na kisiasa maana
mawasiliano yanawezesha na kuhimili sekta nyingine kuongeza ufanisi wa
kiutendaji na kutoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa moja kwa moja na kwa
kupitia sekta za Elimu, Afya, Kilimo, Biashara, Ajira, mabenki, utalii uwekezaji
na sekta nyingine zote kama nyenzo za uwezeshaji katika kuongeza ufanisi wa
kiutendaji”. amesema Mhandisi
Imelda
Aidha Meneja wa TCRA kanda ya ziwa Mhandisi Imelda Salumu ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi wote kuwa
kesi mbalimbali za uhalifu mtandaoni ikiwemo wizi na utapeli zinapaswa
kupelekwa kwenye vituo vya jeshi la Polisi ambao ndiyo wenye jukumu la
kushughulikia kesi hizo na kwamba TCRA haishughulikii kesi za namna hiyo.
Akiwasilisha mada iliyohusu maadili na kanuni za
utangazaji mwandishi wa habari mwandamizi Bwana Edwin Soko amesema usalama wa
mwandishi wa habari unategemea zaidi uzingatiaji wa miiko na maadili katika
kazi yake.
Soko amesisitiza kuhusu uandishi wa habari
unaozingatia ukweli,usawa,na mizania kwa pande zote zinazohusika.
“Sisi
waandishi wa habari tunatakiwa tufanye nini kwenye miiko na maadili yetu,
vyombo vya habari kwanza kabisa tunatakiwa turipoti habari zetu kwa ukweli na
usahihi kwahiyo msingi wa kwanza ni kuwa wakweli tuhakikishe maudhui yetu
hayatuletei shida, maudhui yetu yakiwa yana usahihi na yana mizania tutakuwa
salama zaidi lakini vile vile tuwasilishe jambo ambalo linamantiki ya
kuwasilishwa”.amesema Soko
Kwa upande wake afisa habari na mawasiliano wa TCRA
Bwana Robin Albert Ulikaye amesema kuelekeza uchaguzi wa serikali za mitaa na
uchaguzi mkuu ni vema waandishi wa habari kuendelea kuzingatia kanuni za
uchaguzi wakati wa kutengeneza maudhui.
Ameonya kuhusu uandishi wa habari zinazochangia
kuchochea chuki katika jamiii,na badala yake kujikita kwenye maudhui
yanayozingatia maadili na miiko.
Takribani waandishi wa habari 55 kutoka Wilaya za Kishapu,
Kahama na Shinyanga wameshiriki katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
kanda ya ziwa Mhandisi Imelda Salumu akizungumza kwenye warsha hiyo leo Aprili 9,2024.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
kanda ya ziwa Mhandisi Imelda Salumu akizungumza kwenye warsha hiyo leo Aprili 9,2024.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akiishukuru TCRA kwa kuratibu warsha
hiyo ambayo ni chachu kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akiishukuru TCRA kwa kuratibu warsha
hiyo ambayo ni chachu kwa waandishi wa habari.
Warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
ikiendeleo leo Aprili 9,2024 katika
ukumbi wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.

kanda ya ziwa Mhandisi Imelda Salumu akitoa elimu kuhusu majukumu ya TCRA kwenye warsha hiyo leo Aprili 9,2024.
Mwandishi wa habari mwandamizi Bwana Edwin Soko
akiwakumbusha waandishi wa habari majukumu yao ikiwemo suala la maadili na
kanuni leo Aprili 9,2024 kwenye warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga.
Mwandishi wa habari mwandamizi Bwana Edwin Soko
akiwakumbusha waandishi wa habari majukumu yao ikiwemo suala la maadili na
kanuni leo Aprili 9,2024 kwenye warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga.
Mwandishi wa habari mwandamizi Bwana Edwin Soko
akiwakumbusha waandishi wa habari majukumu yao ikiwemo suala la maadili na
kanuni leo Aprili 9,2024 kwenye warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga.
Warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
ikiendeleo leo Aprili 9,2024 katika
ukumbi wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.
Warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
ikiendeleo leo Aprili 9,2024 katika
ukumbi wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.
Warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
ikiendeleo leo Aprili 9,2024 katika
ukumbi wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.
Warsha ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
ikiendeleo leo Aprili 9,2024 katika
ukumbi wa mikutano wa hotel ya Empire mjini Shinyanga.
Afisa mawasiliano wa TCRA Bwana Robin Albert Ulikaye
akizungumza kwenye warsha hiyo ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
leo Aprili 9,2024.
Afisa mawasiliano wa TCRA Bwana Robin Albert Ulikaye
akizungumza kwenye warsha hiyo ya TCRA na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
leo Aprili 9,2024.
Mwandishi wa habari Salvator Ntandu akizungumza
katika majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Mwandishi wa habari kutoka Kahama FM, Sebastian Mnakaya
akizungumza wakati wa majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Mwandishi wa habari kutoka Azam TV, Kasisi Kosta akizungumza wakati wa majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Mwandishi wa habari Kadama Malunde akiuliza swali wakati wa majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Mkurugenzi msaidizi Radio Faraja FM, Anikazi Kumbemba akizungumza wakati wa majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Mkurugenzi msaidizi Radio Faraja FM, Anikazi Kumbemba akizungumza wakati wa majadiliano ya pamoja na TCRA leo Aprili 9,2024.
Post a Comment