Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa wabunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mkoa wa Shinyanga umekamilika leo Jumatano Julai 30, 2025 katika ukumbi wa Shule ya Wasichana Shinyanga, ambapo wagombea wawili wameibuka na ushindi wa kishindo.
Katika mchakato huo uliowajumuisha wajumbe 1,966 kutoka wilaya za Shinyanga Mjini, Kahama na Kishapu, jumla ya wagombea nane walichuana vikali kutafuta nafasi mbili za ubunge wa viti maalum kupitia chama hicho.
Matokeo ya mwisho ni kama ifuatavyo:
-
Santiel Erick Kirumba – kura 730
-
Christina Christopher Mnzava – kura 719
-
Mwanahamis Munkunda – kura 196
-
Salome Wycliffe Makamba – kura 216
-
Feliter Wilson Buzuka – kura 34
-
Alice Salvatory Kyanila – kura 29
-
Christina Kija Gule – kura 23
-
Queenelizabeth William Maku – kura 19
Post a Comment