Sheikh
wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya ametoa wito kwa waumini wa dini ya
Kiislam Mkoani Shinyanga kutumia sherehe za Idd El Fitri kuchagiza amani na
utulivu kwa watu wote hasa wenye mahitaji.
Akitoa
salamu za Idd El Fitri baada ya swala iliyofanyika katika uwanja wa Sabasaba
Kambarage mjini Shinyanga Sheikh Makusanya amesema ni wajibu wa waumini hao kuwa
chanzo cha faraja na amani kwa jamii nzima akiwataja wagonjwa, wafungwa na watu
wengine wenye uhitaji .
Amehimiza
kutembelea wafungwa, wagonjwa na wale wote wanaohifadhiwa kwenye vituo vya
kulelea ili kuwapa faraja na amani kiroho na kimwili.
“Kwa wewe ambaye ulipata kufunga mwezi mtukufu wa
ramadhan tunatarajia watu wapate manufaa kutoka kwako watu wapate amani kutoka
kwako lakini pia kwa wale ambao wako makabulini wewe utakwenda makabulini
kuwaombea dua lakini kwa ndugu zetu ambao wamefungwa wewe uende kule uwape
faraja uende kule uwaombee dua uwape chakula lakini vile vile wale ndugu zote
tulionao waislam na wasiokuwa waislam tujumuike nao pamoja, kwahiyo wewe kama
wewe iwe ni sehemu ya kuleta amani na utulivu tuwe ni watu wa kuhurumiana hasa
katika siku hii ya leo”.amesema Sheikh Balilusa
Kwa
upande wake kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri BAKWATA Mkoa wa Shinyanga Sheikh
Khamis Balilusa amewakumbusha waumini wa Dini ya kiislam kuendelea kuwa mfano
wa matendo mema na kutojihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na mapenzi ya
Mungu.
“Waislam wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga watambue
siku hii ni siku tukufu ni siku ambayo tunapaswa sisi waislam kutekeleza wajibu
wetu wa kushirikiana kutembeleana na kusaidiana pia tunapaswa tuhakikishe wale
wajane watoto yatima tunawaona na kuwajali ili wapate furaha hasa siku ya leo
lakini pia nitumie fursa hii kuiomba jamii kwamba tujifunze yale yote
yaliyofanyika mwezi mtukufu wa ramadhan kuzidisha wema lakini pia kuhakikisha
sisi waislam kuonya na kujiepusha na tabia mbaya za manyanyaso katika jamii
yetu mauaji mateso kwa watoto na akin a mama pamoja na ubakaji hivi ni vitu
ambavyo waislam naomba wawe kipaumbele kuvisimamia ili kuufanya mji wetu
uendelee kuwa salama na pia uendelee kuwa mji wa amani”.amesema
Sheikh Balilusa
Misalaba
Media imezungumza na baadhi ya waumini wa Dini ya kiislam baada ya swala ya Idd
al Fitri ambao wameahidi kuendeleza utu wema na matendo mema.
Sheikh
wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza swala kwenye ibada ya Idd El
Fitri ambayo imefanyika katika uwanja wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga
leo Aprili 10,2024.
Ibada ya Idd El Fitri ikiendelea katika uwanja
wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga leo Aprili 10,2024.
Ibada ya Idd El Fitri ikiendelea katika uwanja
wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga leo Aprili 10,2024.
Ibada ya Idd El Fitri ikiendelea katika uwanja
wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga leo Aprili 10,2024.
Ibada ya Idd El Fitri ikiendelea katika uwanja
wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga leo Aprili 10,2024.
Post a Comment