Ticker

6/recent/ticker-posts

TIMU MBILI ZATINGA FAINALI, MBILI KUWANIA NAFASI YA TATU MICHUANO YA SALOME MAKAMBA CUP

 

Na Elisha Petro

Timu za Town Stars na Chipukizi FC kutoka kata ya Ngokolo zimefanikiwa kukata tiketi ya kuwania ubingwa wa michuano ya Salome Makamba Cup inayoendelea kurindima Manispaa ya Shinyanga ambapo Town Stars wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya ushindi walioupata dhidi ya Ngokolo Stars na Chipukizi FC wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya ushindi dhidi ya Bugweto FC.

Chipukizi FC wamefanikiwa kufika fainali baada ya kuwatoa Ndala FC kwa ushindi wa goli 4 – 0 katika hatua ya kwanza na kufuzu hatua ya pili ambapo walifanikiwa kuwatoa Home boys FC kwa ushindi wa goli 1 – 0 na kutinga hatua ya tatu ambayo iliwakutanisha dhidi ya Boko FC katika mchezo ulioamuliwa kwa mikwaju ya Penati ambayo iliwapa tiketi Chipukizi FC kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Bugweto FC na kuibuka washindi kwa 1 – 0.

Wakati huohuo, timu ya Town Stars imetinga hatua ya fainali baaada ya kuwatoa Mshikamano FC kwa ushindi wa goli 2 – 0 katika hatua ya kwanza na kutinga hatua ya pili ambapo walikutana dhidi ya Ngokolo Stars na kuibuka na ushindi wa 2 – 1 ushindi uliowapa nafasi ya kuingia hatua ya tatu ambayo walikutana dhidi Mwadui United FC na kupata ushindi wa goli 2 – 0 na kupata tiketi ya kucheza nusu fainali dhidi ya Ngokolo Stars ambapo wamepata ushindi wa mikwaju ya Penati 3 – 0.

Leo Ijumaa ya tarehe 31.05.2024 hatua ya safari ya kumtafuta mshindi wa tatu itaanza kurindima kuanzia majira ya saa 10:00 jioni ambapo wenyeji timu ya Bugweto FC kutoka kata ya Ibadakuli watashuka dimbani kuwakaribisha Ngokolo FC kutoka kata ya Ngokolo katika uwanja wa Bugweto.

Michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Mh. Salome Makamba ambapo zawadi za washindi zitakabidhiwa Jumamosi ya tarehe 01.06.2024 katika uwanja wa Sabasaba uliopo Kambarage mjini Shinyanga, baada ya mchezo wa fainali kumalizika.

Wachezaji wa timu za Bugweto FC na Chipukizi FC wakisikiliza maelekezo kabla ya mchezo kuanza uwanja wa Boko

Wachezaji wa timu za Bugweto FC na Chipukizi FC wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza

Wachezaji viongozi (Captain) katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo

Wachezaji wa timu ya Chipukizi FC katika picha ya pamoja

Wachezaji wa timu ya Bugweto FC katika picha ya pamoja

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo wa nusu fainali kati ya Chipukizi FC dhidi ya Bugweto FC katika uwanja wa Boko

Picha za matukio mbalimbali wakati wa mchezo kati ya Chipukizi FC vs Bugweto FC kwenye uwanja wa Boko

Wachezaji wa Ngokolo Stars wakipasha misuli kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Town Stars kwenye uwanja wa Bugweto

Wachezaji wa Town Stars wakipasha misuli kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ngokolo Stars Stars kwenye uwanja wa Bugweto

Wachezaji wa timu ya Ngokolo Stars katika picha ya pamoja kabla ya mchezo

Wachezaji wa timu ya Town Stars wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo

Waamuzi katika picha ya pamoja na wachezaji viongozi wa timu zote mbili Ngokolo Stars na Town Stars kabla ya mchezo kuanza

Wachezaji wa timu zote mili Town Stars na Ngokolo Stars wakiwa katika picha ya pamoja kupokea maelekezo kabla ya mechi kuanza

Picha za matukio mbalimbali wakati mchezo ukiendelee

Mchezo ukiwa mapumziko ya muda (water break) pembeni waliokaa ni mashabiki wakiendelea kupata burudani

Post a Comment

0 Comments