" WAZAZI NA WALEZI SHULE YA NYAHANGA KAHAMA MKOANI SHINYANGA WAMETAKIWA KUCHANGIA CHAKULA SHULENI ILI KUONGEZA UFAULU KWA WANAFUNZI

WAZAZI NA WALEZI SHULE YA NYAHANGA KAHAMA MKOANI SHINYANGA WAMETAKIWA KUCHANGIA CHAKULA SHULENI ILI KUONGEZA UFAULU KWA WANAFUNZI

Sebastian Mnakaya, Kahama  Wazazi na walezi Halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchangia chakula shuleni kwa wanafunzi ili wasiweze kushinda njaa wawapo darasani pamoja na kuongeza ufaulu.Hayo yamesemwa  na diwani wa viti maalum kata ya Nyahanga HELLEN BUNDALA wakati akiwakabidhi walinu na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyahanga masufuri na vikombe kwa ajili kuanza kupika chakula shuleni hapo, ambapo amesema wazazi kwa kushirikiana wadau wa maendeleo kuchangia huduma hiyo pasipo kusita ili wanafunzi wasishinde njaa shuleni."Nakabidhi masufulia na vikombe kwa walimu na kazi yenu ni kufaulisha na tutaendele kutafuta wafadhili  wa hapa na pale kuhakikisha tunaongeza sufuria na mahitaji mengine ili kutafuta ufaulu wa watoto hao na kuomba wazazi ambao mpaka sasa bado hawajachangia na kuwataka wachange ili huduma hiyo ianze" amesema HELLEN BUNDALAKwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyahanga Maria Saidi na Shabani Songoro wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kutokuwepo kwa chakula shuleni inawasababisha kutokusoma vizuri na kuwaomba wazazi zao kuchangia huduma hiyo ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao." Mara ya kwanza hapa shuleni tulikuwa hatupati chakula mpaka tunaporudi nyumba, ambapo changamoto hiyo inatusababisha kuwa na uchovu hali inayosababisha kutofanya vizur darasan" amesema Maria SaidNae, kaimu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nyahanga Mwalimu PHILIPO KADONO, amesema kuwa ili kuweza kukamilisha upatikani wa chakula shuleni, naomba kutafutwa ufundi ili aweze kujenga jiko kwa ajili ya huduma hiyo huku akimshukuru diwani huyo kwa kuwapatia masufuri na vikombe hivyo kwa ajili kupikia."Niwaombe kwa wale ambao bado hawajachangia huduma hii, wachange ili wanafunzi wapate chakula shuleni ambayo itawasaidia kuongeza ufauli"amesema mwalimu Kadono.Hata hivyo, shule ya sekondari Nyahanga ni shule mpya ya kata ilioazishwa mwaka huu 2024 na imejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi 724 kutoka fedha za serikali kuu, ikiwa na uwezo wa kubeba wananfunzi 780 na kwa sasa inawanafunzi 557 wa kidato cha kwanza.Diwani wa viti maalum Nyahanga akikabidhi sufiria na vikombe kwa wanafunzi wa shule ya secondary Nyahanga.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post