Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga (SPC) Greyson Kakulu akisoma risala leo Mei 15,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
(Shinyanga Press Club) SPC leo Meo 15,2024 imeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo
vya habari Duniani huku ikihamasisha jamii kutunza mazingira ili kusaidia utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati
safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034.
Hafla ya maadhimisho hayo imefanyika katika ukumbi
wa mikutano Karena Hotel na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi
binafsi, vyama vya kisiana, wadau pamoja na baadhi ya wananchi ambapo mgeni
rasmi ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Akisoma risala, Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa
habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakulu pamoja na mambo mengine amesema
klabu hiyo imejipanga kikamilifu katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira ili
kusaidia utekelezaji wa mkakati wa
matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034.
Mwenyekiti huyo amewaomba wadau mbalimbali
kujitokeza kuunga mkono juhudi hizo huku akisisitiza ushirikiano katika maeneo ambayo waandishi wa
habari wa Mkoa wa Shinyanga watayafikia ikiwa ni sehemu pia kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi.
“Tunaposherekea
maadhimisho ya Mwaka huu, vyombo vyetu vya habari vinaweka mtazamo juu ya
mabadiliko ya tabia nchi kwa nia kubwa ya kutoa elimu kwa jamii itakayochochea
uhifadhi na utunzaji wa mazingira”.
“Maadhimisho
ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “uandishi wa habari na changamoto ya
mabadiliko ya tabia nchi” ndugu wadau wa habari: tunahitaji ushirikiano wa
dhati kutoka kwenu kwa ajili ya kampeni ya mazingira ndani ya mkoa wetu “NAFASI
YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA YA MABADILIKO YA TABIA NCHI, kampeni hii
itaendeshwa na vyombo vyetu vya habari kupitia majukwa mbalimbali ili kuhamasisha
jamii yetu kutunza mazingira, kampeni hii itasaidia pia utekelezaji wa mkakati wa
matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034”. amesema
Mwenyekiti Kakulu
“Ndugu
wadau wa habari Waandishi wa habari wanahitaji ushirikiano kutoka kwenu juu ya
habari za mazingira kwa taasisi zote za umma na binafsi katika kutoa elimu na
hata maeneo mengine, Mkoa wetu kwa mwaka 2022 kwa taarifa kutoka Baraza la
Habari Tanzania, ulishika nafasi ya 02 kwa wanahabari kufanyiwa madhira
mbalimbali ikiwa ni kunyimwa taarifa kutoka ofisi za umma na binafsi na hii
ilifanya jamii kukosa haki ya habari kwa maeneo tofauti”.
“Ndugu
wadau wa habari Uhuru wa kujieleza ni uhuru wetu sote bila aina yoyote ya
ubaguzi,Niki mnukuu Katibu wa Umoja wa Mataifa ,Antonio Guteress (Mei 3,2023)
,alisema, Uhuru wetu wote unategemea uhuru wa vyombo vya habari. Tunasomo kubwa
la kujifunza juu ya UVIKO-19, kama vyombo vya habari tungekaa kimya,wengi wetu
hapa tusingekuwa hai hadi leo. Hivyo basi usalama kwa maeneo yote ni uhuru wa
vyombo vya habari”.
“Ndugu
wadau wa habari Nawashukuru sana kwa kutupa ushirikiano kwa vyombo vya habari
kwa mwaka 2023 na mkoa wetu haukuweza kuwa na madhira mengi kama ilivyokuwa huku
nyuma kwa matu”. amesema Mwenyekiti Kakulu
SPC kupitia Mwenyekiti wake Greyson Kakulu
imeishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kufanya marekebisho ya sheria ya kifungu 09 ya sheria ya vyombo vya
habari pamoja na kuongeza uhuru wa kujieleza ambayo pia hivi karibuni
itatekeleza mradi wa UHURU WA KUJIELEZA.
“Ndugu
wadau wa habari Tunashukuru serikali ya awamu ya sita, Mhe.Dkt Samia suluhu kwa
kufanya marekebisho ya sheria ya vifungu 09 ya sheria ya vyombo vya habari na
kuongeza uhuru wa kujieleza”.
“Hivi
karibu klabu yetu itakuwa na mradi UHURU WA KUJIELEZA ambao utakutanisha
kupitia majukwa mbalimbali kwa ajili tena na tutajadili mambo mbali kwa ajili ya
masilahi ustawi wa mkoa wetu, Mradi huu utawapa haki kwenu kama wadau kupaza
sauti juu ya ustawi wa maendeleo ya mkoa wetu katika majukwa mbalimbali”.amesema
Mwenyekiti Kakulu
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi
Macha amewahakikisha waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuwapa
ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwapongeza kwa
kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari 2024.
Pia amesisitiza watendaji wengine wa serikali, taasisi
binafsi pamoja na wadau mbalimbali
katika Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa
ushirikiano kwa waandishi wa habari ili jamii iweze kufahamu changamoto na
maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.
RC Macha amewahimiza waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga kuendelea kutumia kalamu zao vizuri na kutekeleza utekelezaji wa majukumu
yao unazingatia sheria na taratibu
zilizopo ili kuepusha migogoro na upotoshaji katika jamii.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ametumia nafasi hiyo
kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi halali huku akiwaomba
waandishi wa habari kuhamasisha jamii kufanya kazi halali ili kuinuka kiuchumi
na kuepukana na hali utegemezi.
Amewataka waandishi wa habari kuandika Habari kwa kuzingatia Misingi na Kanuni za uandishi wa Habari hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji
Katika maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo
vya habari viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wameshiriki
kujadili mada mbalimbali ikiwemo umuhimu
wa vyombo vya habari katika habari za mazingira, uharibifu wa mazingira na
athari kwa wanawake na watoto pamoja na ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha
akiwapongeza waandishi wa habari Mkoa huo kwa kuadhimisha siku ya uhuru wa
vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga (SPC), Greyson Kakulu akisoma risala leo Mei 15,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha awali
akiwasili ukumbini huku akiongozwa na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa
habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakulu.
Hafla ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya
habari ikiendelea kwa waandishi wa habari, viongozi na wadau mbalimbali Mkoa wa
Shinyanga.

Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake
laki moja Mkoa wa Shinyanga Annaskolastika Ndagiwe ( MC Mama Sabuni)
akizungumza kwenye hafla ya SPC katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo
vya habari Duniani.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Anamringi Macha akikabidhi miche ya miti uliyoandaliwa na SPC ikiwa ni sehemu
ya utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya maadhimishi ya uhuru wa vyombo vya
habari inayosema “uandishi wa habari na
changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi miche ya miti uliyoandaliwa na SPC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya maadhimishi ya uhuru wa vyombo vya habari inayosema “uandishi wa habari na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Patrick Mabula akifunga hafla ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari katika Mkoa wa Shinyanga.

Post a Comment