Daktari wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mohamed Zizimiza akizungumza.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kujitokeza
kwenye kambi maalum ya upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa
yasiyoyakuambukiza inayoendelea katika soko la Ngokolo mitumbani Manispaa ya
Shinyanga.
Wito huo umetolewa na daktari wa magonjwa ya ndani
katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mohamend Zizimiza ambaye
amesema ni muhimu kila mtu kuwa na utamaduni wa kupima ili kufahamu hali ya
afya yake.
Amesema magonjwa yasiyoyakuambukiza yanatokana na
mtindo ambao siyo mzuri wa maisha ambapo amesema kuwa shinikizo la juu la damu
ni tatizo linaloongoza katika takwimu za
wagonjwa wanaohudumiwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
“Ukubwa
wa tatizo la magonjwa yasiyoyakuambukiza kwa takwimu za Dunia ukienda katika
magonjwa kumi (10) ambayo yanasababisha vifo Duniani ni magonjwa matatu yote ya
mwanzo niyasiyoyakuambukiza kwahiyo tukija katika Hositali yetu katika Mkoa
wetu kwa wagonjwa tunaopokea katika wodi zetu pamoja na wagonjwa wanaokuja
Kriniki, wagonjwa wengi tunaopokea ni kutokana na magonjwa hayo
yasiyoyakuambukiza ikiwamo pamoja na shinikizo la juu la damu, kisukari pamoja
na uzito uliokisili”.
“Mara
nyingi unapokuwa na magonjwa yasiyoyakuambukiza changamoto kubwa inatokana na
mtindo usiokuwa mzuri wa maisha ambau unaweza kupelekea kupata uzito wenye
kukisili umbao utasababisha kupata presha ambao ni shinikizo la juu la damu
pamoja na kisukari lakini kwa takwimu za wagonjwa ambao tunawahudumia katika
taasisi yetu tatizo la kwanza ambao linaongoza ni shinikizo la juu la damu ambalo
pia changamoto yake tunayokutana nayo ni kuongezeka kwa wagonjwa ambao wanatatizo
la kiharusi (Stroke)”.
“Wito
wangu kwa wananchi ni kwamba magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ni tishio si
katika nchi yetu pekee yake ni katika Dunia nzima na si tishio tu katika afya
lakini pia katika uchumi wan chi kwa sababu gharama za matibabu za magonjwa
hayo ziko juu sana kwahiyo ninawasihi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo
jirani kuhudhuria katika kambi hii ili kujua hali za afya zao lakini pia kwa
wale ambao wamegundulika wawe na tabia za kuweza kufuatilia hali zao kwa
kuhudhuria kriniki lakini pia kufuata maelekezo na ushauri wa wataalam wa afya”.amesema
Dkt. Zizimiza
Amesema maratajia ya zoezi la upimaji na utoaji wa
elimu ya magonjwa yasiyoyakuambukiza ni kuwafikia wananchi takribani mia tano.
Kwa upande wake afisa habari wa Hospitali ya rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga Bwana George Mganga amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupata
huduma bure za vipimo kwa magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Amesema zoezi hilo linaendelea kutolewa bure ikiwa
ni wiki maalum ya maadhimisho ya shinikizo la juu la damu Duniani, ambayo kauli
mbiu yake inasema ‘Pima shinikizo la damu kwa usahihi, udhibiti, uishi muda
mrefu’ na kwamba kilele chake ni Mei 17, 2024.
Baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wameshukuru
na kupongeza kwa huduma nzuri zinazotolewa katika kambi hiyo huku wakiomba
huduma hizo ziweze kuendelea kutolewa katika maeneo karibu ya wananchi.
Kambi hiyo maalum ni kwa ajili ya upimaji bure wa
magonjwa yasiyoyakuambukiza kama shinikizo la juu la damu (Presha), uzito,
kisukari na elimu ya afya inayohusu magonjwa hayo pamoja na lishe.
‘Huduma katika kambi maalum Ngokolo mitumbani
inatolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi
saa 9:30 alasiri’
Afisa habari wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Bwana George Mganga akiwaomba wananchi kujitokeza kwenye kambi hiyo.
Afisa habari wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Bwana George Mganga akiwaomba wananchi kujitokeza kwenye kambi hiyo.
Mtoa huduma Jesse Samwel akimpima Mama mmoja wa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.
Daktari wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mohamed Zizimiza akiendelea kutoa ushauri kwa wananchi.
Post a Comment