Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwanaume mmoja anayeitwa Shaban Ally mwenye umri wa
Miaka 40 mkazi wa mtaa wa Chamaguha Manispaa ya Shinyanga amefariki Dunia huku unywaji
wa pombe ya kienyeji aina ya Gongo ukitajwa kuwa chanzo.
Tukio hilo limetolea Jumanne Mei 14,2024 na kwamba Misalaba
Media imezungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Chamaguha Bwana Hussein Matamba ambaye
ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa mke wa marehemu.
“Mimi
nilipigiwa simu kwamba kuna tukio hapa
jirani kuna mtu amekufa basi nikaamua nifike pale nimeenda nikakuta kweli yule kijana
anaitwa Shaban Ally amefariki alikuwa ni muuza matunda nikamuuliza mke kwamba
ilikuwaje mpaka kufikia hatua ya kufa mke akasema siku ya Jumatatu marehemu
aliondoka kwenda kwa ndugu zake aliondoka baada ya kumaliza kunywa chai lakini
alikuja kurudi muda wa jioni akapitiliza kulala ndani akiwa anatoka jasho sana
akamsemesha akaona haitikii akasema basi kwa kuwa amelala akapotezea akaendelea
na shughuli zake tu akatoka maana wote huwa niwanywaji wa Pombe sana”.
“Alipokuja
kurudi jioni akamuona yupo tu anajigeuza pale hakumjali nay eye akalala tu,
amelala sasa kuamka asubuhi akamuona bado anahangaika hangaika akamuuliza kwamba
nikukologee uji akakubali na hiyo sauti ya kukubali hakuzungumza tena yule mama
aliendelea kukologa uje akamnywesha kama kikombe kimoja maana alimnywesha akiwa
amelala wakati anaendelea kumnywesha uje akaona mwenzake analainika na kunyoka
badae akajisaidia basi ikiwa umauti ndiyo umemfika kwa namna hiyo”.
amesema Matamba
“Asilimia
kubwa imeonekana Pombe ndiyo imesababisha maana huwa anabishara ya matunda
asubuhi tu utamuona amelewa kwahiyo huwa anakunywa sana hizi Pombe za kienyeji
na mimi huwa nawaambia sana waache hizo Pombe zao lakini vijana wa sasa
hawaelewi”.amesema Matamba
Mwenyekiti huyo amesema baada ya kufika katika eneo
la tukio amechukua hatua za kutoa taarifa hizo katika mamlaka mbalimbali
ikiwemo jeshi la Polisi pamoja na ofisi ya mtendaji wa kata.
Misalaba Media imefanya juhudi za kumpata kaimu
kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga haikufanikiwa.

Post a Comment