Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA FIKRA MPYA LAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 14 HADI 24 KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA

Mkurugenzi wa shirika la Fikra mpya, Leah Josiah akizungumza kwenye maafunzo hayo yanayolenga kuwainua kiuchumi wasichana  wenye umri wa Miaka 14 hadi 24 Manispaa ya Shinyanga.

TAZAMA VIDEO.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Shirika la FIKRA MPYA limetoa mafunzo ya ujasiliamali  kwa wasichana (Mabinti) wenye  umri wa  Miaka 14 hadi 24 ambao wametoka kwenye kata mbalimbali ikiwemo Ngokolo na Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili mjini Shinyanga na kwamba wawezeshaji mbalimbali wametoa elimu ya ujasiliamali na masuala ya ukatili kwa wasichana  ikiwa lengo waimarike kiuchumi.

Mkurugenzi wa shiriki hilo la FIKRA MPYA Leah Daud Josiah amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao kupitia mradi wa “Chaguo langu” ambapo amesema shirika hilo litaendelea kuwasaidia wasichana wenye changamoto mbalimbali wakiwemo waathirika wa ukatili ili waondokane na hali ya utegemezi katika maisha yao ya kila siku.

“Tumekuwa na siku mbili za kujifunza na mabinti ambao wanachangamoto mbalimbali katika maeneo yao wanakoishi ikiwemo kukatishwa masomo kutokana na mimba za utotoni na masuala mengine yanayohusiana na ukatili tumejifunza vitu wengi ndani ya siku hizi mbili ikiwemo masuala ya ujasiliamali yaani tofauti kati ya mjasiliamali na mfanyabiashara lakini pia mbinu mbalimbali za kubaini mawazo ya kijasiliamali pamoja na mikakati ya namna ya kuendesha biashara zao hapo mbeleni kwa kuwa kimekuwa ni kipindi kifupi cha mafunzo ya siku mbili wamejifunza baadhi ya vitu ambavyo vitawasaidia kuondokana na mawazo waliyokuwa nayo ya nyuma na kuingia katika ukurasa mpya wa kujitafuta kama wajasiliamali”.

“Huu ni mradi ambao tunatamani uwe ni mradi endelevu kwa siku zijazo tukiamini kwanza msichana anapojikomboa katika suala zima la kiuchumi anapokuwa mtu ambaye amefanikiwa tunaamini anajiepusha na mazingira yanayomsababishia ukatili kwahiyo sisi wetu Fikra mpya ni faraja, kwanza siku ya pili ya mafunzo yetu wao wamechagua kitu ambacho wanapenda kukifanya ili waweze kufikia malengo yao kwahiyo watajifunza Mwezi mzima wakisaidiwa na wawezeshaji wengine na hiyo ndiyo itakuwa mwendelezo wa mradi wetu wa Changuo langu”.amesema Leah

Afisa maendeleo wa kata ya Ngokolo Bi. Agness Francis amelipongeza shirika hilo kwa kuwapa mafunzo wasichana hao kwa lengo la kuwainua kiuchumi huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

“Mradi huu kwa kweli nimeufurahia na nimshukuru na kumpongeza mkurugenzi wa Fikra mpya kwa utendaji wao wa kazi katika mradi huu lakini pia kwa kuweza kutambua  uwepo wa serikali na kutushirikisha na kwa sababu mradi bado unaendelea naahidi kutoa ushirikiano pale ambapo nitahitajika wasisite kunitafuta lakini pia nitakuwa kipaumbele sana kwa ajili ya kuwasimamia kama serikali na kuhakikisha malengo yao yanafanikiwa”.amesema Agness

Baadhi ya wasichana ambao wamepata mafunzo hayo wamelishukuru shirika la FIKRA MPYA kwa kuwapa elimu ambayo wamesema itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Shirika la FIKRA MPYA ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linatekeleza miradi yake katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine nchini Tanzania ambapo limetoa mafunzo kwa wasichana zaidi ya kumi kwa lengo la kuwainua kiuchumi pia ni sehemu ya utekelezaji wa majumu ya shirika hilo.


Afisa maendeleo wa kata ya Ngokolo Bi. Agness Francis  akizungumza katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la FIKRA MPYA.

Post a Comment

0 Comments