Ticker

6/recent/ticker-posts

AJALI YAUA WATU WATATU BARABARA YA TINDE – KAHAMA

 Watu  watatu  wamepoteza maisha katika ajali ya Barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia jana Jumatatu Julai 1, katika Barabara ya Tinde –Kahama eneo la kijiji cha Puni kata ya Puni,Wilaya ya Shinyanga, Ikihusisha Bus la abiria la kampuni ya Abood kugongana na gari ndogo aina ya NOHA.

Akizungumza na Misalaba Media, Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi  Kenedy Mgani amesema kufuatia ajali hiyo jumla ya watu wanne wamejeruhiwa  ambapo wawili kati yao wamelazwa katika kituo cha Afya cha Bugisi na wengine wawili katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Mwawaza Manispaa ya Sinyanga

Kaimu kamanda huyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ya NOA kuhama upande wake hivyo kugongana uso kwa uso na Bus hilo la Abiria.

Post a Comment

0 Comments