Ticker

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI SHINYANGA KUENDELEA NA UCHUNGUZI WA TUKIO LA MZEE WA MIAKA 70 KUJINYONGA BUGWETO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kufanya uchunguzi katika tukio la Mzee mwenye umri wa Miaka 70 aliyefahamika kwa jina la Christopher Simbila mkazi wa Mtaa Bugweto kata ya Ibadakuli  Manispaa ya Shinyanga, ambaye amejinyonyonga hadi kufa.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Kenedy Mgani, amesema tukio hilo limegunduliwa na  jirani yake ambapo inasadikiwa mzee huyo amejinyonga jana Jumatatu Julai 1, majira ya asubuhi.

Ameeleza kuwa Mzee huyo amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ambayo aliifunga kwenye kenchi Sebleni kwake, hali iliyomsababishia kifo chake papo hapo ,ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa huenda kifo cha mzee huyo kimechangiwa na msongo wa mawazo kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Misalaba Media, imezungumza na Mtoto wa Marehemu Bwana Paul Simbila ambaye ameeleza kuwa jana asubuhi wakati akimpeleka Mtoto wake shuleni, alipita nyumbani kwa Baba yake ili kumtakia hali lakini alipoingia ndani alimkuta akiwa amejinyonga.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto A, Bwana Kulwa Mnyeleshi amesema alipata taarifa baada ya kupigiwa simu na mmoja wa wanafamilia kwamba Mzazi wao amejinyonga nyumbani kwake, ambapo alichukua hatua ya kutoa taarifa polisi.

Jeshi la polisi linatoa wito kwa jamii kuchukua hatua za kuwashirikisha ndugu, jamaa, marafiki au majirani  kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakabili badala ya kuchukua  maamuzi ya kutoa uhai.

Post a Comment

0 Comments