Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma
Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Mtyangimbole leo Jumanne Septemba 24,2024 Mhe. Rais Samia amesema: "Mradi huu unakwenda kuhudumia vijiji vitatu ndio makusudio lakini maji yatabaki, yatakwenda kwenye Kijiji kingine cha nne. Kwa hiyo ndugu zangu nimeona mradi nimeona maendeleo. Nimewaambia Waziri na Katibu Mkuu wake ambao ni wachapakazi wazuri sana na watendaji wao, ninawapa miezi mitatu tu, siku 90 za kazi, mwezi mmoja kufanya yale ambayo mmechelewa kukamilisha, maji yatoke kwa wananchi hawa".
"Mnakumbuka wakati wa kampeni, tuliahidi kumtua ndoo mama kichwani. Sasa tumekwenda kuifanyia kazi ahadi ile. Tumeifanyia kazi kwa kusambaza miradi ya maji nchi nzima. Kama mnavyoona tulivyofanya Ruvuma na nchi nzima ni hivyo hivyo. Kwa hiyo tunatarajia ikifika mwaka kesho 2025 tuwe tumetimiza lile lengo tulilotumwa na Chama Cha Mapinduzi kwamba vijiji vyote vya Tanzania vipate maji kwa asilimia 85 tutakuwa tumelitimiza au kupita kidogo", amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Muonekano wa ujenzi wa Mradi wa maji Mtyangimbole uliopo katika eneo la Kibilang’ombe, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Mtyangimbole uliopo katika eneo la Kibilang’ombe, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma leo Septemba,24 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma leo Septemba, 24 2024.
0 Comments