Benki ya NMB kanda ya Magharibi imekabidhi zawadi kwa wateja wake ambao ni washindi wa kampeni ya BONGE LA MPANGO, yenye lengo la kuwahamasisha wananchi kujiwekea akiba kwenye akaunti zao za NMB ili kukabiliana na dharura mbalimbali na maisha ya baadae.
Hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya mabasi CDT – manispaa ta Kahama mkoani Shinyanga, imewawezesha wateja wawili wa benki hiyo BENARD KIMARO na CHAUSIKU TINDIGA Kukabishiwa zawadi zao ambazo ni trekta la kulimia (pawatila) pamoja na microwave.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, meneja wa NMB kanda ya Magharibi Restus Assenga, ametaja zawadi zinazoshindaniwa katika kampeni hiyo kuwa ni pamoja na fedha taslimu, Friji, TV na pikipiki maarufu kama TOYO yenye magurudumu matatu, mashine ya kufulia, jiko la gesi na trekta la kilimo (power tiller).
“Katika kampeni hii mshindi wa jumla atajishindia kitita cha shilingi milioni 100 taslimu huku kukiwa na zawadi nyingine mbalimbali, na tunaamini kwamba watu wakiwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye akaunti zao, watajiepusha na mikopo umiza (kausha damu) pale wanapopata dharura inayohitaji fedha.” Alisema Assenga
Kila wiki tutakuwa na washindi 10 watakaojishindia shilingi milioni 100 kila mshindi huku washindi 9 wakijishindia kimojawapo kati ya Friji, SmartPhone, TV, mashine ya kufulia na jiko la Gesi.” Aliongeza
Kwa upande wake meneja wa NMB tawi la Kahama Said Pharseko amewasisitiza watanzania kuendelea kujiwekea akiba kupitia benki hiyo ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali.
Joram Mtafya ni mkaguzi wa michezo ya kubahatisha kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, ameirai benki ya NMB kuendesha mchezo huo kwa uadilifu, na kuhakikisha washindi wanaopatikana wanakuwa wamekidhi vigezo vya kushiriki.
Katika hafla hiyo washindi wapya watatu wamepatikana kupitia droo iliyochezeshwa papo hapo, ambapo mshindi wa kwanza kutoka Mwanza amejishindia pawatila (trekta ya kulimia), wa pili kutoka Mwanza pia, amejishindia toyo na watatu kutoka Loliondo - Arusha akijishindia kiasi cha shilingi laki moja.
Mpaka sasa kupitia kampeni hiyo ya ‘BONGE LA MPANGO’ MCHONGO ND’O HUU benki ya NMB imeshakuwa na wshindi 64 walioshinda fedha taslimu, ambapo washindi 60 kati yao walijishindia laki moja moja kila mmoja huku washindi 4 wakijishindia shilingi milioni tano kila mmoja.
‘BONGE LA MPANGO’ MCHONGO ND’O HUU
Post a Comment