“wananchi wamewaamini ndio maana wamewachagua kuwatumikia nendeni mkafanya kazi kwa kushirikiana, Imani yenu kwa wananchi ni kuwatumikia, kuwaletea maendeeo kwenye mitaa yao, pamoja na kutatua changamoto zinazo wakabiri, Uimara wa serikali unatengenezwa na ninyi viongozwa serikali za mitaa rai yangu kwenu nendeni mkafanye kazi kwa kushirikiana na waajiliwa wa Serikali waliopo katika maeneo yenu ya utawala” amesema RC Macha.
Katika hatua nyingine RC Macha ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi hao wa serikali za mitaa, ambapo amewataka kuhakikisha amani inakuwepo katika maeneo yao ya utawala,kusimamia miradi ya maendeleo,pamoja na kutambua mipaka yao ya kiutendaji kazi. kubwa zaidi mkawahimize wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao hatimae taifa kwa Ujumla.
“swala la amani likawe kipaumbele chenu, msiwe chanzo cha migogoro, nendeni mkatatue changamoyo zinazowakabili wananchi hususani migogoro ya aridhi, lakini pia tambueni mipaka yenu ya kazi/utendaji kazi lakinia ujumla” ameongeza Macha.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius R. Kagunze amesema uchaguzi umemalizia kwa amani ambapo Jumla ya Viongozi wa serikali za mitaa 570 wamechaguliwa kutoka vyama hivyo vya siasa , Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishinda mitaa 55, Vijiji 17, Vitongoji 83 Huku Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikishinda kitongiji kimoja pekee cha Mwagala Kata ya Ibadakuli ndani ya manispaa hii. Huku wananakwe wakiwa ni asilimia 30% walio shinda uchaguzi huo
Post a Comment