" WENYEVITI ACHENI KUDHULUMU ARDHI

WENYEVITI ACHENI KUDHULUMU ARDHI

Katavi 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji nchini kuacha kuuza ardhi za wananchi kinyemela ili kuzuia migogoro ya ardhi.

Mhe Pinda amesema hayo leo 29 Novemba 2024 katika hafla ya kuwaapisha wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa serikali za mitaa iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Usevya iliyopo halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi.

Mhe. Pinda meongeza kuwa mwenyekiti hana mamlaka pekee yake ya kuidhinisha mauzo ya eneo isipokuwa kwa kushirikiana na halmashauri ya kijiji  kuuza eneo la ekari zinafikia 50.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi mhe. Mwanamvuaba Mrindoko amesema migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikisababishwa na wenyeviti wa mitaa na vitongoji wasio waadilifu kwa kuwalaghai wananchi ikiwemo kugushi  nyaraka za mauzo ya ardhi.

Aidha mhe. Mrindoko amewataka wenyeviti hao kufanya kazi kwa hofu ya Mungu katika kipindi chao chote cha utumishi wao katika nafasi zao l.

Wenyeviti wote walioapishwa katika hafla wametoka Chama Cha Mapinduzi CCM huku wenyeviti wa vitongoji 654 sawa na 98.8% pia wameshinda nafasi hizo kupitia CCM
 










Post a Comment

Previous Post Next Post