RATIBA MPYA YA MSHINDI WA TATU NA FAINALI KATIKA LIGI YA MAKAMBA LAMECK ( KRISMAS CUP 2024 )
MSHINDI WA TATU
Tarehe: 16 Desemba 2024 (Jumatatu)
Muda: Saa 10:00 jioni
Mechi: Kano FC vs Mwasenge FC
Uwanja wa Mhangu
FAINALI
Tarehe: 18 Desemba 2024 (Jumatano)
Muda: Saa 10:00 jioni
Mechi: Beya FC vs Salawe Stars
Uwanja wa Mhangu
Kwa mujibu wa Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Kijida, mabadiliko haya yamesababishwa na msiba wa bibi wa wachezaji na viongozi zaidi ya sita wa Beya FC, ambapo mazishi yatafanyika Jumanne, tarehe 17 Desemba 2024.
Mwandaaji na mdhamini wa ligi hiyo Bwana Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL, ametoa pole kwa familia ya Beya FC kufuatia msiba wa bibi wa wachezaji na viongozi zaidi ya sita wa timu hiyo.
Mashabiki wote wanahimizwa kuendelea kuonyesha mshikamano na kusapoti timu zao huku wakizingatia ratiba mpya.

Post a Comment