Na Lucas Raphael,Tabora
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amewataka watoa hudumu wa Afya wa Mkoani humo ,kuzingatia ufanisi wa Kazi na kufanya Kazi kwa ushirikiano wawapo kazini ili kutoa huduma Bora kwa wananchi wanaehitaji huduma hiyo ya Afya.
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa JM Hotel mkoani Tabora.
Rugwa alisema bohari ya madawa (MSD) imezidi kuboresha utoaji huduma kwa wadau wake jambo linalochangiwa na kusikiliza maoni na mapendekezo inayopewa kutokana na vikao vinavyofanywa na MSD na wadau wake.
Alisema kuwa majadiliano na kukumbushana majukumu ya kila mmoja yamesababisha huduma zinazotolewa na MSD kuwa bora kila siku.
Alisema kwamba ni lazima ushirikiano uwepo baina ya wateja,wadau ili kuweza kuwafikia wananchi katika kutoa huduma Bora za matibabu.
Alisema kwamba ili kuboresha huduma za afya watenda kazi wanapaswa kufanya kazi kwa umoja kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Tanzania.
Rugwa alibainisha kuwa serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba ambapo wananchi wanapaswa kupata huduma Bora za afya
Alisema bohari ya dawa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kusambaza dawa pindi wanapata uhitaji kutoka hospitali husika.
Awali meneja wa Kanda ya Tabora Rashid Omary alisema kwamba hadi kufikia Aprili mwaka huu kipitia mfumo wa eLmis ulichini ya wizara ya afya imefanikiwa kusajili vituo vya kutolea huduma 793 .
Bohari ya Dawa Kanda ya Tabora inatoa huduma katika Halmashauri 21 na vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya 790 katika mikoa ya Kigoma ,Katavi na Tabora.
Mwisho
Post a Comment